Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Rais wa Colombia Gustavo Petro (kushoto) na Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Luis Acosta/Jim Watson/AFP/Getty Images
Marekani imetangaza siku ya Jumapili kusitisha ufadhili wake kwa Colombia ikitaja kuwa rais wa nchi hiyo Gustavo Petro hachukui hatua za kukabiliana na shughuli za madawa ya kulevya.
Baadaye wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza kuwa ilizishambulia meli kadhaa za Columbia zinazoshukiwa kuhusishwa katika biashara hiyo haramu.
Hayo yanajiri baada ya rais Donald Trump kumtaja Petro kuwa ni mfanyabiashara haramu wa dawa za kulevya huku akimuonya kuchukuwa hatua dhidi ya shughuli hizo kabla ya Marekani kuingilia kati kwa hatua ambazo amesema hazitakuwa nzuri.
Huu ni msuguano wa hivi punde zaidi kati ya Marekani na mmoja wa washirika wake wa karibu katika eneo la Amerika ya Kusini baada ya wiki kadhaa za kurushiana maneno makali. Mwaka 2023, Colombia ilipokea msaada wa dola milioni 740 kutoka Marekani huku nusu ya fedha hizo zikitengewa mamlaka za kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.