Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Mashambulizi ya Israel huko Gaza siku ya Jumapili 19.10.2025Picha: Amir Cohen/REUTERS
Israel imetangaza Jumapili kusitisha mashambulizi yake ya anga katika Ukanda wa Gaza ambayo kulingana na mamlaka za afya yamesababisha vifo vya watu 45.
Jeshi la Israel lilidai kuwa lilishambulia maeneo kadhaa yanayodhibitiwa na Hamas, baada ya wanamgambo wa kundi hilo la Kipalestina kuwashambulia na kuwaua wanajeshi wake wawili huko Rafah, kusini mwa Gaza.
Hamas kwa upande wao wanasema Israel inatafuta sababu za kuanzisha tena mapigano. Pande zote mbili zimekuwa zikitupiana lawama kwa kukiuka mpango huo wa kusitisha mapigano uliosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump na uliodumu kwa siku tisa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.