Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaka Rais Volodymyr Zelensky wa UkrainePicha: Bonnie Cash/UPI Photo/newscom/picture alliance
Rais wa Marekani Donald Trump amemtaka Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine kufikia makubaliano na Urusi wakati alipokutana naye jana Ijumaa katika Ikulu ya Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump amemtaka Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine kufikia makubaliano na Urusi, wakati alipokutana naye jana Ijumaa katika Ikulu ya Marekani. Trump amefifisha matumaini ya Kiev ya kuuziwa makombora ya masafa marefu aina ya Tomahawk huku kiongozi huyo akiongeza juhudi za kuvimaliza vita.
Trump alisema mwezi uliopita kwamba anaamini Ukraine inaweza kurudisha maeneo yake yote, lakini sasa rais huyo anaonekana kubadilisha mwelekeo wake haswa baada ya kukubali kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Budapest huko Hungary.
Baada ya kukutana na Zelensky katika Ikulu ya Marekani, Trump alisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba mazungumzo yao yalikuwa ya kufurahisha sana na ya kupendeza, lakini amemweleza Zelensky kama vile alivyopendekeza kwa Rais Putin, kwamba ni wakati wa kukomesha mauaji, na kufikia makubaliano.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.