Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Mwili wa Raila Odinga unasafirishwa hadi mjini Bondo kwa helikopta ya kijeshi kwa sasa baada ya shughuli ya shughuli ya kumuaga kukamilika mjini Kisumu.
Hatua ya kusafirisha mwili kwa ndege imechukuliwa na kamati ya mazishi ya Odinga kwa ajili ya kuzuia umati mkubwa uliopo Kisumu kuchelewesha mwili huo kufika nyumbani kwake OPODA FARM kwa wakati unaofaa.
Kabla ya kuondoka, mapadri wa kijeshi walisimama na kuomba dua fupi wakati jeneza lilipokuwa linafungwa na maafisa wa jeshi la Kenya.
Kikosi maalum cha makomando wa jeshi la KDF lilizingira mwili na kuulinda vilivyo wakati jeneza lilipokuwa likiondolewa mahali lilipokuwa limewekwa uwanjani kabla ya kuingizwa kwenye ndege hiyo.
Tangu kuwasili Kisumu kwa ndege ya kijeshi aina ya SPARTAN, mwili wa Raila haujasafirishwa kwa barabara japo umekuwa ukisafiri hatua fupi tu kwa kuwa uliwekwa kwa ndege aina ya helikopta na kuseafirishwa hadi uwannja wa mamboleo ambao ulijaa mapaema alfajiri.
Mwili huo utapokelewa na mjane wake Ida Odinga aliyewasili nyumbani mapema leo na wanawe wakiongozwa na Raila Odinga Jr aliyeondoka Mamboleo nusu saa kabla ya mwili wa Baba yake kuondolewa uwanjani humo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.