Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Picha za wanasiasa Tidjane Thiam, Alassane Ouattara na Laurent GbagboPicha: DW
Mamlaka nchini Ivory Coast zimetangaza marufuku ya miezi miwili kwa mikutano ya kisiasa na maandamano, wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais.
Mamlaka nchini Ivory Coast zimetangaza marufuku ya miezi miwili kwa mikutano ya kisiasa na maandamano, wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais. Tangazo hilo, lililotolewa Ijumaa jioni na wizara za mambo ya ndani na ulinzi, linavihusu vyama vyote vya kisiasa kasoro tu wagombea watano walioidhinishwa rasmi kuwania uchaguzi wa Oktoba 25.
Kumekuwa na ongezeko la mvutano kufuatia kuondolewa kwa wanasiasa vigogo Laurent Gbagbo na Tidjane Thiam kushiriki uchaguzi. Muungano wa upinzani, unaojumuisha chama cha Gbagbo cha PPA-CI na kile cha Thiam cha PDCI, umelaani juhudi za Rais Alassane Ouattara kuwania muhula wa nne.
Mamia ya watu waliandamana mwishoni mwa juma lililopita mjini Abidjan huku vikosi vya usalama vikitawanya umati. Vurugu zimeripotiwa katika mikoa chungu nzima ikiwa ni pamoja na kuzuia barabara na shule.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.