Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Mwili wa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga unaagwa kitaifa leo Ijumaa kwa ibada maalamu mjini Nairobi na kuhudhuhuriwa na viongozi wakuu na wawakilishi wa serikali mbalimbali duniani.

Mwili wa Raila Odinga ulipowasili nchini Kenya siku ya Alhamisi ukitokea India.Picha: Andrew Kasuku/AP Photo/picture alliance
Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa ibada hiyo itafanyika kwenye uwanja wa michezo wa Nyayo na kuongozwa na Rais William Ruto wa nchi hiyo.
Odinga, mwanasiasa kigogo wa upinzani aliaga dunia siku ya Jumatano akiwa nchini India alikokwenda kwa matibabu.
Mwili wake ulirejeshwa nyumbani jana Alhamisi na maelfu ya watu walipata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye uwanja wa Kasarani nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.
Hata hivyo zoezi hilo lilikumbwa na vurumai iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua watatu ya baada ya polisi kufyetua risasiili kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wakisongamana kuelekea jukwaa la watu mashuhuri.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.