‘Mfalme amekufa, lakini taji lake liishi milele’: Winnie Odinga amuaga Raila

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader
.

Winnie Odinga, bintiye aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Odinga, amtoa pongezi kwa babake na kumueleza kuwa “Baba na shujaa” ambaye upendo, akili na ujasiri vilibadilisha maisha yake.

“Sijui nitamkosa nani zaidi – Baba yangu au shujaa wangu,” alianza, huku waombolezaji wakisikiliza kwa makini.

“Mimi ndiye msichana mwenye bahati zaidi duniani kwa sababu ulikuwa Baba yangu.

Ni binadamu wengine watatu tu walikuwa na bahati kama mimi Fidel, Rozzy na Junior.

“Winnie alimuelezea baba yake kama mwanga mwepesi “usiobadilika na binadamu wa kina” ambaye uwepo wake uliamsha usikivu popote alipoenda.

“Kwa ulimwengu, ulijulikana kwa majina mengi,” alisema. “Hata ulimpa karibu kila mtu uliyekutana naye jina la utani pia.

Lakini kwangu, ulikuwa tu Baba

“Alikumbuka kwa moyo mkunjufu maisha yao ya nyumbani, ambayo aliyataja kuwa “mahali pa kufanyia majaribio vitendawili,” ambapo Raila angewapa watoto wake changamoto na mafumbo na yaliwafungua akili .

“Nyumba yetu ilijaa maswali ambayo yalitujaribu kwa njia nzuri… wakati mwingine,” alisema huku akitabasamu kidogo. Winnie alisema alicheka aliposikia kuhusu nia ya mwisho ya babake kutaka kuzikwa ndani ya saa 72 baada ya kifo chake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment