Guterres alaani jeshi kuchukua madaraka nchini Madagascar

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Madagascar baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umma dhidi ya utawala wa Rais Andry Rajoelina.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Picha: Jason DeCrow/AP/picture alliance

Guterres amekosoa mabadiliko ya uongozi yasiyozingatia katiba na ametoa mwito wa kurejea kwa utawala wa kiraia chini ya msingi wa katiba.

Matamshi yake ameyatoa wakati kanali wa jeshi  aliyechukua madaraka siku ya Jumanne Michael Randrianirina anatarajiwa kuapishwa leo Ijumaa kuwa rais wakati wa halfa itakayofanyika katika majengo ya Mahakama ya Juu ya Katiba kwenye mji mkuu, Antananarivo.

Umoja wa Afrika pia umelaani mapinduzi hayo na kuisimamisha Madagascar uanachama wake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment