Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


‘Baba nataka kukuhakikishia kuwa nitatunza familia yetu…. Asante kwa kunipa jina lako…’
“Nafahamu kwa hakika kwamba kaka yangu Fidel hayupo tena, mimi ndio mwanamume wa familia. Baba, nataka kukuhakikishia kwamba nitatunza familia yetu – Mama, Rosie, Winnie – na familia kubwa ya kisiasa ambayo umeiacha … asante kwa kunipa jina lako na kamwe hukuwahi kunipa uzito wa jina hilo.” – Raila Odinga Jr.
‘Mfalme amekufa, lakini taji lake liishi milele’: Winnie Odinga amuaga Raila
Winnie Odinga, bintiye aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Odinga, amtoa pongezi kwa babake na kumueleza kuwa “Baba na shujaa” ambaye upendo, akili na ujasiri vilibadilisha maisha yake.
“Sijui nitamkosa nani zaidi – Baba yangu au shujaa wangu,” alianza, huku waombolezaji wakisikiliza kwa makini.
“Mimi ndiye msichana mwenye bahati zaidi duniani kwa sababu ulikuwa Baba yangu.
Ni binadamu wengine watatu tu walikuwa na bahati kama mimi Fidel, Rozzy na Junior.
“Winnie alimuelezea baba yake kama mwanga mwepesi “usiobadilika na binadamu wa kina” ambaye uwepo wake uliamsha usikivu popote alipoenda.
“Kwa ulimwengu, ulijulikana kwa majina mengi,” alisema. “Hata ulimpa karibu kila mtu uliyekutana naye jina la utani pia.
Lakini kwangu, ulikuwa tu Baba
“Alikumbuka kwa moyo mkunjufu maisha yao ya nyumbani, ambayo aliyataja kuwa “mahali pa kufanyia majaribio vitendawili,” ambapo Raila angewapa watoto wake changamoto na mafumbo na yaliwafungua akili .
“Nyumba yetu ilijaa maswali ambayo yalitujaribu kwa njia nzuri… wakati mwingine,” alisema huku akitabasamu kidogo. Winnie alisema alicheka aliposikia kuhusu nia ya mwisho ya babake kutaka kuzikwa ndani ya saa 72 baada ya kifo chake.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.