Buriani Raila Odinga: Ibada ya wafu ya mwili wa ‘Baba’ yaendelea uwanjani Nyayo

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Wakenya hususan wale wanaoishi Mjini Nairobi hii leo siku ya Ijumaa watapata fursa ya kuuaga mwili wa Raila Odinga kwa siku ya pili mfululizo katika uwanja wa Nyanyo Jijini Nairobi baada ya ibada ya mazishi.

Na:Cantona Joseph|RFA

Buriani Baba: Mwili wa Raila kuagwa kwa siku ya pili Nairobi baada ya ibada ya mazishi

.

Wakenya hususan wale wanaoishi Mjini Nairobi hii leo siku ya Ijumaa watapata fursa ya kuuaga mwili wa Raila Odinga kwa siku ya pili mfululizo katika uwanja wa Nyanyo Jijini Nairobi.

Hatua hii inajiri baada ya Serikali Kutangaza siku kuu ya Raila siku ya ijumaa ili kutoa fursa ya kuuaga mwili wa marehemu.

Kulingana na ratiba ya mazishi iliotolewa na serikali, Kutakuwa na na ibada ya mazishi mapema leo kabla ya mwili wake kuagwa.

Naibu rais Kithure Kindiki anayeongoza ratiba ya mazishi ya kiongozi huyo maarufu nchini Kenya amesema kwamba Wageni ikiwemo viongozi wa mataifa jirani Afrika na wale wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Amewasihi Wakenya kuwasili katika uwanja huo mapema zaidi kuanzia saa tatu asubuhi ili kuzuia ghasia kama zile zilizoshuhudiwa katika uwanja wa kasarani.

Siku ya Alhamisi watu watatu wlifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika machafuko yaliyozuka katika uwanja wa Kimataifa,

Kasarani, ambapo maelfu ya Wakenya walikuwa wamekusanyika kutoa heshima zao za mwisho

Buriani Baba: Wabunge kumuaga Raila Odinga katika majengo ya Bunge

.

Ratiba ya mazishi ya Raila Odinga imebadilika kwa mara nyengine hii leo baada ya mwili wake kupelekwa hadi bunge ili kuagwa na viongozi hao.

Mwili huo uliotarajiwa kusafirishwa moja kwa moja hadi katika uwanja wa Nyayo, ulipelekwa bungeni ili kuwapa fursa wabunge kuuaga kabla ya kupelekwa katika uwanja wa Nyayo.

Hapo Jana ratiba hiyo ilibadilika kwa mara ya kwanza baada ya waombolezaji kuupokea mwili wake katika uwanja wa ndege wa JKIA na kutembea nao moja kwa moja hadi Kasarani ili kuagwa.

Hii ilikuwa kinyume na ratiba hiyo ambapo ulitarajiwa kuchukuliwa kutoka JKIA , kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee kabla ya kupelekwa bungeni ili kuagwa.

Mwili huo sasa utaagwa bungeni ambapo rais atawaongoza viongozi tofauti kuuaga mwili huo.

Inasemekana kuwa wabunge waliombwa kuwa maeneo ya bunge mapema leo kwa ajili ya kumuaga.

Baadaye mwili huo utapelekwa katika uwanja wa Nyayo ambapo ibada ya mazishi itafanyika kuanzia saa 9 asubuhi kabla ya Wakenya kupewa fursa nyengine kuuaga

Buriani Baba: Tazama Wakenya wakimsubiri Raila uwanjani Nyayo

Maelezo ya video,Buriani Baba: Wakenya waendelea kuwasili uwanjani Nyayo

Wakenya wameshawasili katika uwanja wa michezo wa Nyanyo kwa ajili ya ibada ya kitaifa ya kumuaga aliyekuwa Waziri Mkuu nchini Kenya Raila Odinga.

Usalama umeimarishwa nje na ndani ya uwanja wa Nyayo na kwa sasa wafuasi wa Raila wanaimba na kucheza.

Kulingana na ratiba, wananchi wanatakiwa kuwa wameketi kufikia saa mbili asubuhi.

Mwili wa Raila Odinga tayari umeshatolewa katika Makafani la Lee na umefikishwa kwenye majengo ya bunge kwa ajili ya wabunge na viongozi wengine kumuaga.

Inatarajiwa kuwa baada ya bunge, moja kwa moja utapelekwa katika uwanja wa nyayo kwa ibada ya kitaifa ya kumuaga.

Raila Odinga aliaga dunia alipokuwa anapata matibabu nchini India.

Maelezo ya video,Buriani Baba: Wakenya wawasili uwanjani Nyayo

Briani Odinga: Wakenya wazidiwa na hisia katika ibada ya kumuaga Raila

.

Wakenya wazidiwa na hisia baada ya kuwasili kwa mwili wa Raila Odinga katika uwanja wa Nyayo kwa ajili ya kuagwa.

Uwanja ulijaa vilio na huzuni huku wengine wakiwa tayari kuufuata mwili wakati unazungushwa kwenye uwanja. Hata hivyo, ulizinzi umeimarishwa

Kwa Picha, tazama Wakenya wakimuomboleza Raila Odinga.

Buriani Raila Odinga: Mwili wa ‘Baba’ wawasili uwanjani Nyayo kwa ibada ya wafu na kuagwa

.

Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga umewasili Nyayo kwa Mazishi ya Kitaifa.

Msafara wake ulivuka barabara kuu ya Uhuru hadi uwanjani mwendo wa 9:46m.

Gari la maiti lilipoingia polepole, waombolezaji waliangua vilio, kabla ya kuzunguka katka uwanja huo.

Mwili huo ulikuwa umeondoka kwenye Majengo ya Bunge kuelekea Uwanja wa Taifa wa Nyayo, kuashiria awamu inayofuata katika mazishi ya serikali.

Msafara huo ulianza muda mfupi baada ya saa 9:20 asubuhi, huku wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na bendera nje ya lango kuu la Bunge.

Mlinzi wa sherehe za heshima alisimama makini huku gari la kubebea maiti, lililozungukwa na maafisa waliovalia sare na wanafamilia, likipitia barabara za Nairobi.

Umati wa watu ulijipanga njiani, wengi wakipeperusha bendera, vijiti, na kushikilia picha za marehemu.

Wengine walilia hadharani, wengine waliimba nyimbo ambazo zilirejelea mapambano ya miongo kadhaa ya Raila ya demokrasia na mageuzi.

Baadhi ya waombolezaji walipeperusha bendera na vijiti, alama za maombolezo, huku wengine wakiwa na mabango na picha za kiongozi huyo aliyepewa jina Baba kwa upendo.

Mke wa Raila Odinga, Ida Odinga awasili uwanjani Nyayo

Mke wa Raila Odinga Ida Odinga amewasili katika uwanja wa Kimataifa wa Nyayo.

Tayari msafara wa kijeshi ulibeba mwili wa Raila Odinga uko njiani kuelekea uwanjani Nyayo.

Ibada ya kumuaga Raila kuanza muda mfupi ujao.

Rais Ruto na Viongozi wakuu Serikalini wawasili uwanjani Nyayo

Rais William Ruto anaongoza maelfu ya Wakenya katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi katika ibada ya wafu ya marehemu Raila Odinga.

Aidha aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta , naibu rais Kithure Kindiki , jaji Mkuu Martha Koome ni miongoni mwa viongozi mbalimbali ikiwemo wale wa kimataifa wanaohudhuria hafla hiyo.

Baada ya ibada hiyo Wakenya waliohudhuria hafla hiyo watapata fursa ya kuuaga mwili wa marehemu

Mwili wa Raila Odinga wapelekwa katika uwanja wa michezo wa Nyayo

Mwili wa Raila Odinga sasa umetoka kwenye maeneo ya Bunge kuelekea kwenye uwanja wa michezo wa Nyayo kwa ibada ya kitaifa.

Mwili huo umebebwa na gari la kijeshi na unalindwa na wanajeshi.

Wabunge wameshawasili katika uwanja huo.

Muda mfupi ujao ibada ya kitaifa ya kumuaga inatarajiwa kuanza.

Buriani Raila Odinga: Aliyekuwa waziri Mkuu aagwa Bungeni

.

Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, umeagwa bungeni.

Wabunge na viongozi wengine serikalini wamepata fursa ya kumuaga.

Na sasa jicho limeelekezwa kwa ibada ya kitaifa inayofanyika uwanja wa Nyayo.

Rais William Ruto awasili bungeni

Rais William Ruto amewasili katika majengo ya bunge kuungana na viongozi wengine kumuaga Raila Odinga.

Ratiba ya kumuaga Raila inaendelea.

Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, ulipelekwa bungeni kabla ya ibada ya kitaifinayofanyika leo kwenye uwanja wa Nyayo.

Uchimbaji wa kaburi la Raila Odinga unaendelea

.

Uchimbaji wa kaburi la Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga katika makazi ya kijijini ya Bondo unaendelea.

Waziri mkuu wa zamani atazikwa Jumapili nyumbani kwake mjini Bondo.

Kupitia vyombo vya habari vya ndani, trekta ilionekana ikichimba kaburi pale ambapo Raila Odinga atazikwa.

Shughuli hii ilianza baada ya Seneta wa Siaya Oburu Odinga ambaye ni kaka mkubwa wa Raila Odinga kufunguwa rasmi nyumba ya Bondo ya Raila kwa waombolezaji, kuwajulisha rasmi wanakijiji kuwa wamepatwa na msiba na kuonyesha sehemu ambayo kaka yake atazikwa katika eneo la makaburi ya kwao kama sehemu ya desturi ya jamii la luo.

Awali, kulikuwa na tetesi kuwa Raila Odinga alitaka kuzikwa karibu na mama yake Mary Juma lakini ndugu yake Oburu Odinga, ameonyesha sehemu ambayo ndugu yake atazikwa ambako ni kando ya baba yake, Jaramogi Oginga Odinga, kwenye eneo la makuburi ya kwao la Ang’oka Jaramogi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment