Ujerumani yaahidi kitita cha dola bilioni 2 kwa Ukraine

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius.Picha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images

Na:Cantona Joseph|RFA

Ujerumani imeahidi kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 2 mwaka unaokuja ili kuiwezesha kuendelea kuikabili Urusi katika vita vikavyoingia mwaka wa nne.

Tangazo la msaada huo limetolewa na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius mjini Brussels siku ya Jumatano baada ya kukutana na mwenzake wa Ukraine Denys Shmyhal.

Waziri Pistorius amesema wa Ujerumani utatumika kununua silaha za karibu dola milioni 500 kutoka Marekani na kuipatia Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga, rada za kijeshi na makombora.

Wawili pia walitia saini mkataba wa kuongeza ushirikiano wa kiulinzi unaojumuisha masuala ya utafiti na maendeleo ya teknolojia.

Ahadi hiyo ya msaada wa kijeshi imetolewa katika wakati serikali mjini Kyiv imesema itahitaji angalau dola bilioni 120 kwa mwaka 2026 zitakazoisadia kuwa na uwezo wa kuendelea kukabiliana na Urusi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment