Rais Rajoelina athibitisha kuikimbia Madagascar

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina alipolihutubia taifa mara baada ya kuikimbia nchiPicha: Rijasolo/AFP/Getty Images

Na:Cantona Joseph|RFA

Rais wa Madagascar aliyeondolewa madarakani Andry Rajoelina amethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba aliikimbia nchi hiyo kati ya Oktoba 11 na 12 kufuatia alichotaja kuwa vitisho vya wazi kwa uhai wake.

Jeshi ambalo lilitangaza kunyakua madaraka limetangaza kuwa kiongozi wao Kanali Michael Randrianirina ataapishwa rasmi siku ya Ijumaa kuwa rais mpya wa Madagascar.

Jumuiya ya kimataifa inapinga hatua hiyo na imewataka wadau wote wa Madagascar kutafuta suluhisho la amani linaloheshimu katiba ya nchi hiyo.

Vuguvugu linaloongozwa na vijana wa Gen Z lilianzisha maandamano makubwa mnamo Septemba 25 kutokana na uhaba wa maji na kukatika kwa umeme huku vijana hao wakimshinikiza rais  Rajoelina  kujiuzulu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment