Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Rais Vlamidir Putin wa Urusi alipokutana na mwenzake wa Syria Ahmed al-Sharaa mjini Moscow Oktoba 15, 2025.Picha: Sergei Bobylev/TASS/picture alliance
Na:Cantona Joseph|RFA
Rais Vlamidir Putin wa Urusi amekutana na kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa mjini Moscow siku ya Jumatano.
Ametumia mazungumzo yao kuusifu uhusiano kati ya nchi hizo mbili hata baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar al-Assad aliyekuwa mshirika mkubwa wa Urusi.
Hiyo ilikuwa ziara ya kwanza ya Al-Sharaa nchini Urusi tangu alipochukua hatamu za uongozi nchini Syria kwa kuongoza uasi ulioungusha utawala wa Assad, Disemba mwaka jana. Assad alikimbia Urusi na kuomba hifadhi ya kisiasa.
Viongozi hao wawili walizungumzia hatma ya kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria pamoja na ushirikiano kwenye sekta za uchumi na maendeleo hususani nishati, uchukuzi na utalii.
Putin amesema Syria inapitia kipindi kigumu lakini uchaguzi wa bunge uliofanyika hivi karibuni umeimarisha ushirikiano baina ya makundi ya kisiasa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.