Polisi wawatawanya waombolezaji kwa vitoa machozi uwanjani Kasarani

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader
Waombolezaji wamefurushwa uwanjani na maafisa wa polisi nchini Kenya
Maelezo ya picha,Waombolezaji wamefurushwa uwanjani na maafisa wa polisi nchini Kenya

Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waombolezaji waliokusanyika katika uwanja wa Kasarani, baada ya hali ya msongamano na mvutano kuibuka.

Hii ni baada ya mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kufikishwa katika Uwanja huo ili umma wampatie heshima ya mwisho.

Ni idadi hiyo ya waombolezaji ambayo ilijaza uwanja huo wa Kasarani unao uwezo wa kuhimili zaidi ya mashabiki elfu hamsini .

Kwasasa shughuli nzima ya kuuona mwili wa kigogo huyo wa siasa Raila Oding imesitishwa ghafla hii ni baada ya shughuli hiyo kusitishwa awali katika bunge la kitaifa la Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari nchini humo, baadhi ya waombolezaji walionekana wakirusha mawe eneo la wageni maalum wakitaka kushinikiza kuuona mwili wa Raila uliokuwa umehifadhiwa hapo.

Ripoti kutoka eneo hilo zinaonesha kuwa kumetokea mkanyagano na watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya.

Katika hali ya kutuliza rabsha maafisa wa polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya waombolezaji ambayo walikuwa wamejaa mlangoni na kupelekea kukimbia kujikinga na hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika vurumai hiyo.

Tamaduni zaanza baada ya kakake Raila Odinga kuwasili Bondo

Hema lawekwa katika eneo ambalo mwili wa Raila utaagwa kabla ya kuzikwa
Maelezo ya picha,Hema lawekwa katika eneo ambalo mwili wa Raila utaagwa kabla ya kuzikwa

Maandalizi yanaendelea kwa ajili ya shughuli ya kuuaga mwili wa Raila Odinga siku ya Ijumaa katika uwanja wa Jomo Kenyatta, Mamboleo.

Awali, shughuli hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika mjini Kisumu.

Eneo hilo litakuwa na maeneo maalum ya kuingilia na kutoka ili kudhibiti msongamano.

Dkt. Oburu Odinga, kaka yake Raila na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Mazishi, amewasili nyumbani kwa Raila huko Bondo, Kaunti ya Siaya.

Kwa mujibu wa utaratibu wa jamii ya Wajaluo, ujio wake unaashiria kuwa boma limefunguliwa rasmi kwa waombolezaji na kwamba familia imetangaza rasmi kifo cha ndugu yao.

Oburu amekutana na wazee wa mtaa, jamaa wa familia, marafiki wa karibu wa Raila, pamoja na viongozi wa kidini ili kuweka misingi ya maandalizi ya mazishi.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kwa mujibu wa taratibu za Kanisa la Anglikana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment