Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Na:Cantona Joseph|RFA
Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waombolezaji waliokusanyika katika uwanja wa Kasarani, baada ya hali ya msongamano na mvutano kuibuka.
Hii ni baada ya mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kufikishwa katika Uwanja huo ili umma wampatie heshima ya mwisho.
Ni idadi hiyo ya waombolezaji ambayo ilijaza uwanja huo wa Kasarani unao uwezo wa kuhimili zaidi ya mashabiki elfu hamsini .
Kwasasa shughuli nzima ya kuuona mwili wa kigogo huyo wa siasa imesitishwa ghafla hii ni baada ya shughuli hiyo kusitishwa awali katika bunge la kitaifa la Kenya.
Maelfu wafurika uwanja wa Kasarani kumuaga Raila Odinga

Maelfu ya waombolezaji wanaendelea kumiminika katika uwanja wa kitaifa wa Kasarani kutoa heshima zao za mwisho kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Raila Odinga.

Viongozi wa matabaka mbali mabi pia wamefika katika uwanja huo kusubiri mwili wa kiongozi huyo wa wa muda mrefu wa upinzani nchini Kenya kufikishwa katika uwanja huo.

Baadhi ya waombolezaji walioenda kuulaki mwili huo katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta wanatembea kuelekea uwanjani hapo.
Kwa sasa msafafara huo uko kwenye barabara kuu ya Thika kuelekea uwanja wa Kasarani.
Kwanini ratiba ya kuuaga mwili wa Raila Odinga Bungeni ilibadilishwa?
Machafuko yalizuka nje ya majengo ya Bunge jijini Nairobi wakati waombolezaji walipojaribu kuingia kwa nguvu katika jengo hilo ili kusubiri kuwasili kwa mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenye Raila Odinga.
Hali iligeuka kuwa ya vurugu wakati maelfu ya wafuasi, waliokuwa wamekusanyika kando ya Barabara ya Bunge, walipovunja vizuizi vya vilivyowekwa kando ya barabara ya City Hall.
Walipanda juu ya lango, wakiimba nyimbo za ukombozi na kulia kwa majonzi.
Maafisa wa usalama walijitahidi kuzuia umati uliokuwa ukiendelea kufurika, huku waombolezaji wakijitahidi kufikia lango la kuingia majengo ya bunge.
Baadhi walionekana wakisukuma lango hilo kwa nia ya kulivunja huku baadhi ya waombolezaji wakipanda kwenye milango na ua wa Bunge wakipeperusha matawi na bendera hewani wakiomba waruhusiwe kuingia.
Oburu Oginga ateuliwa kaimu kiongozi wa chama cha ODM
Seneta wa Siaya Oburu Oginga ameteuliwa kuwa kaimu kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kufuatia kifo cha mdogo wake Raila Odinga.
Odinga, kiongozi wa muda mrefu wa chama hicho, alifariki siku ya Jumatano nchini India, ambako alikuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haukutajwa.
Wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Alhamisi asubuhi, chama kilikubaliana kwa kauli moja kwamba Oginga achukue uongozi wa chama hadi kamati hiyo itakapokutana tena kupanga mustakabali wake.
Rais William Ruto ametangaza siku saba ya maombolezo ya kitaifa, ambapo bendera ya Kenya itapeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Odinga atazikwa siku ya Jumapili huko Bondo, Kaunti ya Siaya magharibi mwa Kenya.
Shughuli ya kutazama mwili wa Raila Odinga imehamishwa hadi uwanja wa Kasarani

Shughuli ya kutazama mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Amollo Odinga imehamishwa kutoka maeneo ya Bunge hadi uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani, baada ya umati mkubwa wa watu waliokusanyika nje ya majengo ya bunge kufanya iwe vigumu shughuli hiyo kuendelea kama ulivyopangwa.
Mipango ya awali ya kupeleka mwili wa Raila Odinga kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) hadi makafani ya Lee kwa ajili ya matayarisho ya mwisho kabla ya kupelekwa kutazamwa na umma ilifutiliwa mbali huku kukiwa na ongezeko la machafuko ya umati.
Maafisa wa kijeshi na waandalizi wa maiti waliokuwa wametumwa katika kituo cha makafani cha Lee kupokea na kuandaa mwili huo badala yake wameagizwa kuelekea Kasarani, ambako shughuli hiyo sasa itafanyika.
“Umati wa watu haukuweza kudhibitiwa. Waandalizi wa maiti na timu yake wameondoka kwa gari la kijeshi,” afisa mkuu wa Hifadhi ya Maiti ya Lee aliwaambia waandishi wa habari.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.