Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Pakistan na Afghanistan zimetangaza kusitisha mapigano baada ya siku kadhaa za makabiliano makali ya mpaka ambayo hayajapata kushuhudiwa kwa miaka mingi iliyopita.

Mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan yametishia kuzuka vita kamili.Picha: Sanaullah Seiam/AFP
Na:Cantona Joseph|RFA
Taarifa ya usitishaji mapigano imetolewa na nchi zote mbili ingawa kila upande umesema ombi la kusimamisha mapigano lilitolewa na mwenzake.
Duru zinasena uamuzi huo umefikiwa kufuatia miito kutoka mataifa yenye ushawishi kwenye kanda hiyo, ikiwemo Qatar na Saudi Arabia.
Mapigano kati mataifa hayo jirani yamesababisha vifo vya makumi ya watu na kujeruhiwa wengine kadhaa tangu yalipozuka wiki za karibuni.
Pakistan inaituhumu Afghanistan kutoa hifadhi kwa makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa mipaka yake madai ambayo watawala wa Taliban wamekuwa wakiyakanusha.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.