Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasili mahakamami kusikiliza kesi za ufisadi zinazomkabiliPicha: Yair Sagi/REUTERS
Na:Cantona Joseph|RFA
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amerejea tena Jumatano katika mahakama ya Tel Aviv kusikiliza kesi ya ufisadi inayomkabili na iliyoanzishwa Mei mwaka 2020.
Netanyahu alionekana mwenye tabasamu wakati yeye na msafara wake wa mawaziri kadhaa kutoka chama chake cha kihafidhina cha Likud walipokuwa wakizomewa na waandamanaji wakati wakielekea mahakamani.
Katika moja ya kesi, Netanyahu na mkewe Sara, wanatuhumiwa kupokea bidhaa za kifahari zenye thamani ya zaidi ya dola 260,000, zikiwemo shampeni, sigara na vito kutoka kwa mabilionea waliokuwa wakitaka kupewa upendeleo wa kisiasa.
Kesi hii ya inayomkabili Netanyahu inajiri siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kupendekeza kwamba Waziri Mkuu huyo wa Israel anapaswa kusamehewa katika kesi zake tatu tofauti za ufisadi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.