Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


i. Utakosa nidhamu ya muda
ii. Utahisi kila wakati una mambo mengi yasiyoisha
iii. Utakosa hamasa ya kufanya mambo muhimu
iv. Utakosa ari ya kufanya mambo kwa haraka
v. Utakuwa ni mtu usiye na vipaumbele maishani
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Kwanza Ya Udhaifu
– Utakosa nidhamu ya muda
Sehemu ya kwanza ambayo utadhoofishwa na ambayo itakusababishia uwe na…
…tabia ya kughairisha mambo isiyoisha katika maisha yako ni nidhamu ya muda.
Kwa ufupi, kuwa na nidhamu ni ile hali ya kufanya…
…jambo ulilokusudia bila kujali kama unajisikia kufanya ama la.
Kwa maneno mengine kuwa na nidhamu maana yake ni kuwa…
…unapoamua kufanya jambo fulani basi unalifanya bila kughairisha kwa sababu zozote zile.
Watu ambao mfumo wao wa limbic huwa unawatawala zaidi ni…
…watu ambao kwanza huwa wanapoteza muda sana.
Ni watu ambao hawajali muda wao na wako tayari kuutumia vibaya…
…bila kujali kuwa ukipoteza muda wako basi hautakurudia tena.
Ni kwa sababu ya kutojali muda ndio maana watu wa namna hii wako tayari kughairisha mambo kila saa…
…bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo wanajichelewesha kufanikiwa waliyokusudia kuyafanya.
Katika yale Hebu jichunguze, wewe huwa unajali muda wako ama huwa unautumia muda vibaya?
Kadiri unavyokuwa mtumiaji mbaya wa muda ndivyo ambavyo unakuwa mghairishaji zaidi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.