Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga afariki dunia

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga afariki dunia nchini India akiwa na umri wa miaka 80Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Na:Cantona Joseph|RFA

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amefariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo nchini India.

Hospitali ya Devamatha katika jimbo la Kerala imethibitisha taarifa za kifo chake hivi leo. Odinga ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 80, aliwahi kugombea urais wa Kenya mara tano katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu. 

Mwezi machi,  Raila Odinga  alikuwa amesaini makubaliano ya kisiasa na rais wa sasa William Ruto ambayo yalikiruhusu chama chake cha upinzani cha ODM kushiriki katika mchakato muhimu wa kupitisha sera huku baadhi ya wanachama wake wakiteuliwa kuwa mawaziri.

Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa na kukitangaza rasmi kifo cha Odinga. Viongozi mbalimbali duniani wameanza kutuma salamu zao za rambirambi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment