Rais wa Syria Sharaa kuzuru Moscow Jumatano

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa anatarajiwa kuzuru Moscow leo kwa mazungumzo kuhusu mustakabali wa vituo vya kijeshi vya Urusi nchini humo na hatma ya Bashar al-Assad, aliyepinduliwa mwaka jana na kupewa hifadhi na Urusi.

Rais wa Syria atajadili na viongozi wa Urusi kuhusu uwepo wa vituo vya kijeshi vya taifa hilo nchini Syria, pamoja na hatma ya Bashar al-Assad.Picha: LOUAI BESHARA/AFP/Getty Images

Na:Cantona Joseph|RFA

Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa anatarajiwa kuzuru Moscow Jumatano, kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Syria na chanzo cha serikali kilichonukuliwa Jumanne, licha ya kusogezwa mbele kwa mkutano wa kilele wa Kiarabu aliokuwa akitarajia kuhudhuria.

Chanzo cha serikali kimesema Sharaa atafanya mazungumzo kuhusu mustakabali wa uwepo wa vituo vya kijeshi vya Urusi – bandari ya Tartous na kituo cha anga cha Hmeimim – vilivyobaki nchini humo tangu enzi za utawala wa Bashar al-Assad.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Asaad al-Shibani, akipeana mkono na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, wakati wa ziara yake ya kwanza mjini Moscow tangu kuondolewa madarakani kwa Bashar al-Assad, Julai 31, 2025.Picha: Shamil Zhumatov/Pool Reuters/AP/picture alliance

Kuomba kumkabidhi Bashar al-Assad

Aidha, Sharaa anatarajiwa kuwasilisha ombi rasmi kwa Urusi kumkabidhi Assad, aliyepinduliwa na kupewa hifadhi ya kisiasa mjini Moscow, ili afikishwe mahakamani kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya wananchi wa Syria.

Sharaa, ambaye hapo awali aliwahi kuongoza tawi la al-Qaeda nchini Syria kabla ya kujiunga na waasi waliouteka mji wa Damascus mwezi Desemba, sasa anaendesha serikali mpya ambayo Urusi imejaribu kuendeleza uhusiano nayo kupitia diplomasia na msaada wa kijeshi kufuatia mashambulizi ya Israel nchini humo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment