Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Na:Cantona Joseph|RFA
Katika kipindi cha ujana, una nguvu, ndoto na muda wa kufanya mambo makubwa
Lakini mafanikio hayatokani na juhudi zako pekee yanategemea pia aina ya watu walioko karibu nawe.
Hakikisha kwenye mzunguko wako (circle) UNA WATU HAWA 10 muhimu watakaokusaidia kupanda ngazi moja hadi nyingine…
…
1. MTU WA AFYA
Huyu ni mtaalamu atakayekushauri kuhusu afya yako ya mwili na akili.
Afya njema ndiyo msingi wa mafanikio, bila afya, hata malengo yako yatayeyuka.
Kuwa na daktari, mtaalamu wa lishe, au mtu anayekuhamasisha kuishi maisha yenye afya.
…
2. MTU WA SHERIA
Kuna wakati utahitaji ushauri wa kisheria au ulinzi wa haki zako.
Mwanasheria mzuri atakusaidia kuepuka matatizo ya kisheria na kukutetea pale unaponewa au kudhulumiwa.
…
3. MTU MWENYE HOFU YA MUNGU (ENEO LA KIROHO)
Kuna nyakati mbinu zote za kibinadamu zitashindwa kufanya kazi.
Utahitaji mtu wa kukuinua kiroho, mtu wa maombi, anayekutia imani, na kukukaribisha karibu na Mungu.
Anaweza kuwa mchungaji, shehe, au mtu yeyote mwenye maisha ya kiroho thabiti.
…
4. MTU MWENYE HEKIMA NA BUSARA
Huyu ni mtu wa kukushauri, kukuongoza, na kukupa mwanga wa maisha unapokutana na changamoto.
Hekima yake inaweza kukuepusha na makosa makubwa na kukuokoa muda mwingi wa maisha.
..
5. WATU WALIOKUZIDI KIPATO
Usizunguke tu na watu walio chini yako.
Kaa karibu na wale walioko juu yako kifedha au kimaendeleo watakuvuta juu na kukuonyesha njia ya kufikia ngazi ya juu zaidi.
….
6. WATU WENYE MAMLAKA AU NGUVU YA USHAWISHI.
Kwenye maisha, kuna milango ambayo haifunguki bila mtu mwenye mamlaka.
Kuwa na watu kama hawa katika mzunguko wako wanaoweza kusaidia unapokwama.
Mfano…viongozi wa serikali, watu wa mfumo (system), TRA, RTO, diwani, n.k.
…
7. MTU MWENYE MAARIFA YA KIDIGITALI (DIGITAL INFLUENCER)
Dunia ya leo iko mtandaoni.
Huyu mtu atakusaidia kukuza biashara yako, jina lako, au huduma zako kupitia mitandao ya kijamii.Atakufundisha namna ya kutumia teknolojia kuvutia wateja na kujijenga kiusoni.
….
8. WATU WANAOKUTIA MOYO ( Mentor)
Kuna siku utaishiwa nguvu, matumaini, na motisha.
Hawa ndio watu watakaokutia moyo, kukuhamasisha, na kukukumbusha kwa nini ulianza.Wanakuinua unapokata tamaa.
…
9. WATU WENYE CONNECTION
Kuna watu ambao simu moja tu kutoka kwao inaweza kubadilisha maisha yako.
Watu wa aina hii hufungua milango ya fursa kazi, biashara, au ushauri muhimu.
Usiogope kujenga mahusiano na watu wenye mitandao mizuri.
…
10. WATU WENYE UZOEFU
Hawa wamepita kule unapokusudia kwenda.
Watakusaidia kuepuka makosa, kupoteza muda, na kutumia rasilimali zako kwa ufanisi.
Usianze kutumia watu hawa kabla hujajenga uhusiano wa kweli nao.Waheshimu, shiriki kwenye shughuli zao, kuwa sehemu ya furaha na changamoto zao.
Ukaribu hujenga uaminifu na ndipo msaada wao utakuwa wa dhati.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.