FAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA PESA UKIWA NDANI YA AJIRA.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Kuwa na kazi si tatizo tatizo ni kubaki kutegemea chanzo kimoja cha kipato.

Kazi ni baraka, lakini haipaswi kuwa mwisho wa ndoto zako za kifedha.

Hapa kuna njia rahisi unazoweza kutumia kutengeneza pesa hata ukiwa bado umeajiriwa.

1. TUMIA UJUZI WAKO NJE YA KAZI.

Kama una ujuzi fulani kazini kama uandishi, uhasibu, graphic design, social media, IT, au ushauri wa biashara. Unaweza kuuza huduma hizo kwa watu wengine nje ya muda wa kazi.

Tumia majukwaa kama Facebook, au hata WhatsApp na Instagram kutangaza huduma zako.

2.ANZISHA BIASHARA NDOGO YA PEMBENl.

Huhitaji mtaji mkubwa kuanza.

Anza na kitu kinachouzwa kirahisi na hakihitaji uwepo wako muda wote

mfano bidhaa za mtandaoni, chakula ofisini, bidhaa za nyumbani, nguo, au vipodozi.Fanya biashara inayoendana na ratiba yako ya kazi.

3. WEKEZA SEHEMU YA MSHAHARA WAKO (Passive Income)

Usitumie kila kitu unachopata

wekeza sehemu kidogo kila mwezi kwenye Unit Trusts / Mutual Funds, Hisa / Bonds, REITs (Real Estate Investment Trusts),Kilimo cha mkataba au miradi inayoendeshwa na wengine

Lengo ni pesa yako iifanyie kazi wewe, hata ukiwa kazini.

4. TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KIBIASHARA.

Mitandao si ya kufuatilia watu pekee ni soko kubwa.Anza kutengeneza content ya thamani kulingana na ujuzi wako.

Unaweza kuuza bidhaa, kutoa mafunzo, au kushirikiana na brands.

Kila post inaweza kuwa fursa ya kipato.

5.TOA MAFUNZO AU USHAURI (Coaching Mentorship)

Kama una uzoefu katika taaluma yako, watu wako tayari kulipia maarifa hayo.

Tumia muda wa jioni au wikendi kutoa mafunzo kwa vijana au watu wanaoanza taaluma hiyo.Hii inaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato na heshima.

6. FANYA AKIBA INAYOLETA FAIDA.

Badala ya kuweka hela benki bila faida, tumia njia za akiba zenye riba au miradi midogo yenye mzunguko wa haraka.

Usiweke pesa tu, iweke ikuzalishe.

7. JIFUNZE KUDHIBITI MUDA NA NIDHAMU.

Changamoto kubwa kwa waajiriwa ni ukosefu wa muda.Hivyo, jifunze kupanga siku zako. Amka mapema, tumia jioni kwa miradi yako midogo, na acha muda upotee kwenye vitu visivyozalisha.

ANGALIZO:Usiache kazi yako ili uanze kutafuta pesa anza kutengeneza pesa ukiwa kwenye kazi uliyo nayo..Wengi wamepotea kwa kuacha kazi ghafla usiingie kwenye mkumbo huo.

Tumia kipato chako cha sasa kama ngazi ya kujijenga kifedha.

Ni mbinu gani unahitaji ufafanuzi zaidi kati ya hizi 7.?

Au ni mbinu gani wewe umeitumia kujiongezea kipato ukiwa ndani ya ajira.?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment