Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Na:Cantona Joseph|RFA
Mteja anapofika kwenye biashara yako, hiyo ni nafasi muhimu ya kukuza biashara na kujenga uhusiano wa kudumu. Fuatilia mambo haya 7 ili kupata matokeo makubwa..
…
1. MPOKEE KWA UKARIMU
Simama, tabasamu na mpe salamu ya karibu.Ukarimu wa mwanzo hujenga picha chanya ya huduma zako na humfanya mteja ajisikie kuthaminiwa.
…
2. MSIKILIZE KWA UMAKINI.
Weka kando simu au shughuli nyingine.
Toa muda wako wote kumsikiliza ili kuelewa kwa kina hitaji au changamoto yake.
Mteja anapojisikia kusikilizwa, anaongeza imani na utayari wa kushirikiana nawe.
…
3..KUWA NA TABASAMU LA KAWAIDA.
Tabasamu lina nguvu kubwa kuliko matangazo makubwa.
Linaondoa hofu, linavunja ukuta wa mawasiliano, na linamfanya mteja ajisikie nyumbani.
…
4.TOA SULUHISHO SAHIHI.
Baada ya kuelewa hitaji lake, toa suluhisho kwa weledi na kwa haraka.
Msaidie kuchagua bidhaa/huduma sahihi na hakikisha inatatua changamoto yake.
Jali muda wa mteja kwa kutoa huduma yenye ufanisi bila kuchelewesha.
…
5. FUATILIA BAADA YA HUDUMA.
Baada ya mauzo au huduma, mfuate mteja kuuliza kama amefurahia huduma au bidhaa.
Hii inaonyesha kujali, na huongeza uwezekano wa yeye kurejea tena au kukurejelea wateja wapya.
…
6. DUMISHA UBORA KILA SIKU.
Huduma bora haipaswi kuwa tukio la bahati iwe tabia.Wafundishe wafanyakazi wako kuheshimu kila mteja, bila kujali ukubwa wa mauzo.
..
7.MSHUKURU NA JENGA UHUSIANO.
Usimwache mteja aondoke bila kumshukuru.
Mwambie kwa maneno ya moyo..Asante kwa kuchagua huduma/bidhaa zetu, karibu tena.
Kumbuka, ameacha maduka mengi na kukuchagua wewe, hivyo thamini uamuzi wake.Chukua mawasiliano yake ili kuendelea kumsaidia na kujenga uhusiano wa kudumu.
Ukizingatia haya mambo saba, utajenga jina la biashara yako, kuongeza mauzo, na kupata wateja wa kudumu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.