Biden na Clinton wamsifu Trump kwa kusitishwa vita Gaza

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Marais wa zamani wa Marekani Joe Biden na Bill ClintonPicha: Patrick Semansky/REUTERS

Na:Cantona Joseph|RFA

Marais wa zamani wa Marekani Joe Biden na Bill Clinton wamechukua hatua nadra ya kumsifu Rais Donald Trump kwa kusaidia katika usitishwaji wa vita vya Gaza.

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, Biden amesema kwa kuungw amkono na Marekani na washirika wake duniani, Mashariki ya Kati kwa sasa iko katika mkondo wa kupatikana kwa amani.

Biden vile vile amezungumzia dhima ya utawala wake katikamazungumzo ya amani akisema walijitahidi kuhakikisha wanamgambo wa Hamas wamewaachia mateka, kufikisha misaada kwa Wapalestina na kuvisitisha vita hivyo vilivyoanza wakati wa utawala wake mwaka 2023.

Clinton kwa upande wake amesema Trump,Qatar na wahusika wengine wa kikanda waliopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita wanastahili pongezi kubwa.

Ametaka Israel na wanamgambo wa Hamas wadumishe amani ya kudumu.

Clinton amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump akidai sera zake zinatokana na nia za kibinafsi na wala si maslahi ya raia wa Marekani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment