Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Na:Cantona Joseph|RFA
Huwezi kuwa mtu wa tofauti kama una unaogopa kuwa tofauti.
Dunia imejaa watu ambao wanataka mfanane kwa kila kitu.
Na mara utakapoonyesha kuwa unakitu au mbinu ya tofauti, wanaanza kukugeuza kuwa adui.
Umeshawahi kusikia msemo wa kiswahili unasema “Kifo cha wengi ni harusi?”
.
Kuna wengi sana wanaumini na wanauishi msemo huu.
Kwa sababu hiyo huwa wanatamani kama wao wanapata shida basi kila mtu apate shida.
Kama wao hawana furaha basi kila mtu asifurahi…
.
Kama wao wameshindwa kitu basi kitu mtu ashindwe.
Haujawahi kumuona mtu anakuchukia Kwa sababu ya ulivyo tofauti?
Haujawahi kukutana na mtu anakusema vibaya kwa sababu unaonekana una furaha kila siku?
.
Au haujaona watu wanakutungia uzushi kwa chuki tu Kwa sababu umeamua kuwa mtu wa tofauti?
.
Hii ni gharama ambayo lazima uilipe katika safari yako ya kuelekea kwenye kilele cha ndoto yako.
Kama unaogopa kuwa tofauti huwezi kufanya mambo ya makubwa.
Kuna wakati inabidi ukubali kutoleweka leo ili uelekeweke kesho.
Kuna watu wanawaweza wasikuelewe leo ila wakakuelewa kesho.
Mtu mmoja aliwahi kusema “Kama unataka kupendwa na kila mtu basi usiwe kiongozi, nenda kauze ice-cream”.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.