Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Paul Biya ndiye rais mwenye umri mkubwa zaidi dunianiPicha: Robert Fimbaye/AFP
Na:Cantona Joseph|RFA
Raia wa Cameroon walipiga kura Jumapili katika uchaguzi unaotarajiwa kumrejesha madarakani Rais Paul Biya mwenye miaka 92, ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miongo minne.
Raia wa Cameroon walimiminika vituoni Jumapili kushiriki katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kumrejesha madarakani Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92 na ambaye ndiye kiongozi mzee zaidi duniani anayehudumu kwa sasa. Hali ya upigaji kura ilielezewa kuwa tulivu, huku vituo vingi vya kura katika mji mkuu Yaoundé vikipokea idadi kubwa ya wapiga kura kabla ya kufungwa jioni.
Rais Biya, ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1982, alikabiliwa na wagombea 11, wakiwemo Issa Tchiroma Bakary, waziri wa zamani wa ajira mwenye umri wa miaka 79, aliyevutia umati mkubwa wa vijana katika kampeni. Wataalamu wa siasa wanasema licha ya shauku ya mabadiliko, mfumo wa sasa wa kisiasa una uwezo mkubwa wa kuhakikisha matokeo yanampendelea Biya.

Issa Tchiroma Bakary ameibuka kuwa mshindani mkuu wa BiyaPicha: Daniel Beloumou Olomo/AFP
Vijana wahamasika kwa matumaini ya mabadiliko
Kampeni za uchaguzi huu zimekuwa na mvuto zaidi kuliko chaguzi zilizopita, huku vijana wakiweka matumaini mapya ya mabadiliko kupitia sanduku la kura. Wengi wao wamekuwa wakilalamikia gharama kubwa za maisha, ukosefu wa ajira na huduma duni za kijamii, hali inayochochea kutoridhika na uongozi wa muda mrefu wa Biya.
Tume ya Uchaguzi imesema zaidi ya wachunguzi 55,000 wa ndani na kimataifa, wakiwemo wa Umoja wa Afrika, walisimamia uchaguzi huo. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa ifikapo Oktoba 26, huku baadhi ya majukwaa ya mtandaoni yakiahidi kuchapisha matokeo yao binafsi — hatua ambayo serikali imeikosoa kwa madai ya kujaribu kupotosha maoni ya umma.
Tutumie maoni yako
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.