Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, katikati, atakutana na waziri mkuu wa India, Narendra Modi.
Picha: Leon Neal/Pool via REUTERS
Na:Cantona Joseph|RFA
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer atakutana na waziri mkuu wa India, Narendra Modi mjini Mumbai. Viongozi hao wanatarajiwa kuzungumzia uhisiano na Vladimir Putin.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake ya kibiashara nchini India.
Mjadala kumhusu rais Vladimir Putin wa Urusi huenda ukawa kwenye ajenda ya mazungumzo hayo.
Kando na mkataba mpya wa kibiashara kati ya mataifa yao mawili, Starmer na Modi wanatarajiwa kujadili uhusiano wa kiongozi huyo wa India na Urusi na kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu kwa raia wa Uingereza Jagtar Singh Johal.
Starmer hadi sasa amekataa kujibu maswali kuhusu mahusiano ya karibu kati ya Modi na Putin, na hatua ya India kuendelea kununua nishati ya mafuta kutoka kwa Urusi wakati wa ziara yake Mumbai.
Wakati huo huo, familia ya Jagtar Singh Johal, kutoka Dumbarton, karibu na Glasgow, wanamtaka Waziri Mkuu Starmer kuchukua “hatua madhubuti” ili kupata kuachiliwa kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 38 katika mazungumzo yake na Modi.
Starmer amesisitiza kuwa serikali inawasilisha kesi ya mfungwa huyo katika “kila ngazi.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.