Misri yafuzu kwa kombe la dunia 2026

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mo Salah ameisaidia timu yake taifa ya Misri kufuzu kwa kombe la dunia 2026

Na:Cantona Joseph|RFA

Misri imefuza kwa mashindano ya kombe la dunia la kandanda 2026 kwa kukandika Djibouti 3-0 Casablance.

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah alifunga mabao mawili na kuisaidia Misri kuishinda Djibouti 3-0 mjini Casablanca Jumatano na kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026. Ushindi wa Misri umewapa uongozi usio na kifani wa pointi tano dhidi ya Burkina Faso katika Kundi A.

Wakati Misri wameshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara saba, hawajafanikiwa katika Kombe la Dunia, wakiwa wamefuzu mara nne tu katika majaribio 15 — mnamo 1934, 1990, 2018 na sasa 2026.

Kiungo wa zamani wa Arsenal Thomas Partey alikuwa miongoni mwa wafungaji mabao wakati Ghana ilipoilaza Jamhuri ya Afrika ya Kati 5-0 mjini Meknes, na wanahitaji pointi moja kutoka kwa mechi yao ya mwisho ya Kundi I wakiwa nyumbani dhidi ya Comoro ili kufuzu. Ghana wana alama 22 na tofauti kubwa ya mabao kuliko Madagascar, ambao wako nyuma kwa pointi tatu.

Mali ambayo ilipigiwa upatu kuibuka kidedea katika kundi hilo, iko nje ya michuano hiyo ikiwa na pointi 15.

Katika mechi nyingine Cape Verde ilitoka nyuma kwa mabao mawili mjini Tripoli na kutoka sare ya 3-3 na Libya na kukaribia kufuzu kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment