Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kumtaja waziri mkuu mpya wa Ufaransa–Picha: Jean-Christophe Verhaegen/AFP/dpa/picture alliance
Na:Cantona Joseph|RFA
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamteua waziri mkuu mpya katika kipindi cha saa 48 zijazo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamteua waziri mkuu mpya katika kipindi cha saa 48 zijazo.
Hayo yamesemwa na ofisi yake Jumatano, baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu anayeondoka Sebastien Lecornu kuashiria nchi hiyo kuingia katika mzozo wa kisiasa.
Awali Lecornu aliiambia televisheni ya Ufaransa katika mahojiano kwamba alitarajia waziri mkuu mpya kutajwa — badala ya uchaguzi wa mapema wa wabunge kuitishwa au Macron kujiuzulu — katika jitihada za kuutatua ufumbuzi mgogoro huo.
Jumatatu wiki hii Macron alimpa Lecornu hadi Jumatano jioni kutafuta njia ya kutoka kwa kipindi kigumu cha miezi kadhaa ya msuguano juu ya bajeti ya kubana matumizi.
Lecornu alijiuzulu mapema Jumatatu baada ya kuwa madarakani kwa chini ya mwezi mmoja.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.