Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza wakati wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 24, 2025.
Na:Cantona Joseph|RFA
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameituhumu Urusi kwa kutaka kuleta machafuko barani Ulaya kwa kutumia droni kwa ajili ya hujuma na kuvuruga hali ya usalama.
Katika hotuba yake ya jioni ya Jumanne kwa njia ya video, Zelensky amesema serikali ya Moscow inatumia kile alichokiita “msafara wa kivuli” si tu kufadhili vita kupitia usafirishaji wa mafuta kwa meli kubwa, bali pia kwa hujuma na juhudi mbalimbali za kuvuruga utulivu barani Ulaya. Kurushwa kwa droni kutoka kwenye meli hizo ni mfano mmoja wa hali hiyo.
Hata hivyo taarifa rasmi kuhusu asili ya droni zilizogunduliwa hivi karibuni katika mataifa kama Denmark na Ujerumani bado hazijathibitishwa.Na Urusi imekanusha kuhusika kwa namna yoyote.Dmitry Medvedev, naibu mkuu wa baraza la usalama la taifa la Urusi, alionesha kuwa huenda majeshi ya Ukraine yenyewe ndiyo yanayotumia droni hizo kwa makusudi ili kuichochea Ulaya iingie vitani dhidi ya Urusi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.