Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Andry Rajoelina |Rais wa Madagascer
Na:Cantona Joseph|RFA
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema anapanga kufanya “mazungumzo ya kitaifa” na makundi mbalimbali leo hii, baada ya waandamanaji vijana kumpa saa 48 akubali madai yao au wakaitisha maandamano ya kitaifa.
Amesema kuwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika mchana yatashirikisha viongozi wa kiroho, wanafunzi, wawakilishi wa vijana, na makundi mengine.Jumatatu, Rajoelina alimteua Jenerali wa Jeshi Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya, wiki moja baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake wote katika hatua ya kushughulikia malalamiko yaliyochochea maandamano ya Septemba 25.
Hata hivyo, mabadiliko hayo hayajawatuliza waandamanaji ambao awali walijitokeza mitaani kulalamikia uhaba wa maji na umeme katika taifa hilo maskini la Afrika, lakini sasa wanataka Rais Rajoelina ajiuzulu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.