Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Polisi nchini Tanzania wakishika doria wakati wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa
Na:Cantona Joseph|RFA
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema linafanya uchunguzi kufuatia taarifa kwamba aliyewahi kuwa balozi na ambaye sasa ni mkosoaji wa serikali, Humphrey Polepole, ametekwa.
Familia yake imedai kuwa Polepole alichukuliwa kwa nguvu kutoka nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Kaka yake, Godfrey Polepole, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa nduguye, aliyejiuzulu kama balozi wa Tanzania nchini Cuba mwezi Julai na ambaye amekuwa akikikosoa chama tawala, CCM, alitoweka nyumbani kwake jijini Dar es Salaam mapema Jumatatu.
Tukio hilo limeibua hofu miongoni mwa wakosoaji wa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kugombea tena urais katika uchaguzi wa Oktoba 29.
Tangu mwaka jana, baadhi ya wakosoaji wa serikali wamepotea, huku vyama vya upinzani vikidai kuwepo kwa kampeni ya utekaji nyara.
Msemaji wa serikali, Gerson Msigwa, hakupatikana kutoa maoni baada ya juhudi za kumtafuta kupitia njia ya simu na ujumbe kushindikana.
Katika taarifa iliyotolewa Septemba 29, serikali ilikanusha madai ya shirika la Human Rights Watch kwamba inawakandamiza wakosoaji wake kuelekea uchaguzi mkuu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.