Papa awataka maaskofu kuzungumzia sera za uhamiaji za Trump

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV amewataka maaskofu wa Marekani kuzungumzia sera kali za Rais Donald Trump kwa wahamiaji.

Papa ameyasema haya wakati akizungumza na maaskofu hao waliokuwa wamemtembelea huko Vatican Jumatano.

Hili ni shinikizo la hivi karibuni la kiongozi huyo wa kidini katika suala hilo.

Wakati wa mkutano na maaskofu hao na wafanyakazi wa kijamii kutoka mpaka wa Mexico na Marekani, Papa Leo ambaye ndiye kiongozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki kutoka Marekani, alikabidhiwa dazeni kadhaa za barua kutoka kwa wahamiaji zinazoelezea hofu yao ya kurudishwa makwao chini ya sera za utawala wa Trump.

Ikulu ya Marekani, White House inasema Trump alichaguliwa kutokana na ahadi zake nyingi alizotoa ikiwemo kuwarudisha makwao wahamiaji haramu. 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment