Mashambulizi ya Urusi na Ukraine yasababisha vifo vya watu 5

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwanajeshi wa Urusi akipewa mafunzo ya kutumia silaha

Na:Cantona Joseph|RFA

Mashambulizi kati ya Ukraine na Urusi katika pande zote mbili Jumatano yamesababisha vifo vya watu watano.

Haya ni kwa mujibu wa mamlaka za nchi hizo. Gavana wa jimbo la Belgorodnchini Urusi linalopakana na Ukraine, amesema kombora la Ukraine jimboni humo limesababisha vifo vya watu watatu katika kijiji cha Maslova Pristan, kilichoko umbali wa kilomita 15 kutoka mpakani.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema mashambulizi ya Ukraine nchini mwake hayatosaidia kwa vyovyote katika vita hivyo.

“Adui licha ya majaribio kadhaa ya upinzani, anajiondoa kutoka eneo lote la mpakani. Na kutokana na hili, utawala wa Kyiv, ambao unataka sana kuonyesha mafanikio kwa wafadhili wake wa Magharibi, unajaribu kuwashambulia raia ndani ya Urusi. Hili halitosaidia kamwe,” alisema Putin.

Wakati huo huo, shambulizi la Urusi katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson,limewauwa watu wawili. Haya ni kulingana na gavana wa eneo hilo Vyacheslava Gladkov.

Urusi imerusha takriban droni 183 katika eneo la Ukraine kati ya Jumanne na Jumatano.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment