Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri Mkuu wa muda Ufaransa sebastian Lecornu
Na:Cantona Joseph|RFA
Waziri Mkuu wa muda wa Ufaransa Sebastian Lecornu Jumatano amesema kuwa uwezekano wa kuvunjwa wa bunge la nchi hiyo ni mdogo kwa sasa, baada ya kufanya mazungumzo na vyama tofauti vya kisiasa.
Lecornu anasema kuna nia ya pamoja ya kupitisha bajeti kufikia mwishoni mwa mwaka. Waziri Mkuu huyo anasema atakutana na Rais Emmanuel Macron baadae Jumatano kujadiliana kuhusu matokeo ya mazungumzo yake na vyama hivyo vya kisiasa.
Awali waziri mkuu wa zamani na mwandani wake wakati mmoja Edouard Philippe alikuwa amemtaka Rais Macron ajiuzulu.
Philippe amesema uchaguzi nchini humo unastahilikuandaliwa mara tu bajeti itakapopitishwa.
Uchaguzi ufuatao nchini Ufaransa ambao mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia Marin Le Pen anaona ana nafasi nzuri zaidi ya kuchukua mamlaka unatarajiwa kufanyika mwaka 2027, huku Macron akiwa hawezi kugombea tena urais, na Philippe akiwa tayari ashatangazwa kuwa mgombea.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.