Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Wajasiriamali wengi huanza biashara wakiwa na matumaini makubwa, lakini ndani ya miezi michache mambo hubadilika.
Takwimu zinaonyesha kuwa biashara nyingi hufa kabla hazijafikisha miezi 6,si kwa sababu wamiliki hawana bidii, bali kwa sababu wanakosa misingi sahihi ya uendeshaji. Kuwa makini katika haya..
…
1. KUTOKUFANYA UTAFITI WA SOKO
Wengi huanza biashara bila kujua kama kuna wateja wa kutosha, washindani, au mahitaji halisi ya bidhaa wanazouza.
Matokeo yake: wanauza kitu ambacho watu hawahitaji au tayari kipo sokoni kwa bei ndogo zaidi.
…
2. KUTOKUA NA MPANGO WA FEDHA
Biashara nyingi hufa kwa sababu hazina bajeti, rekodi za mapato na matumizi, au mpango wa mtiririko wa fedha (cash flow).
Wanafikiri wanafaidika kumbe pesa inazunguka tu bila faida halisi.
..
3. KUTOFANYA MATANGAZO YA KUTOSHA
Wajasiriamali wengi huanza kimya kimya wakidhani “ubora utajitangaza wenyewe”.
Ukweli: kama watu hawajui kuhusu biashara yako, hawatanunua — hata kama bidhaa ni bora sana.
…
4. KUTOKUJITOFAUTISH.
Biashara nyingi zinauza kile kile, kwa njia ile ile, bila utofauti wowote.
Matokeo yake, wateja huchagua biashara yenye bei ya chini au jina kubwa zaidi.
..
5. KUKOSA UVUMILIVU NA MPANGILIO
Baada ya miezi michache bila faida kubwa, wengi huanza kukata tamaa na kuacha.
Wanasahau kuwa kila biashara inahitaji muda kukua, kutambulika na kupata wateja wa kudumu.
…
6. HUDUMA MBOVU KWA WATEJA
Biashara nyingi hazina mawasiliano mazuri na wateja hawajibu meseji, hawafuatilii maoni, au wanakuwa wakorofi.
Wateja hawarudi, na bila wateja wa kurudi, biashara inakufa.
…
7. KUTOKUJIFUNZA AU KUBADILIKA
Soko hubadilika haraka, lakini baadhi ya wafanyabiashara hubaki pale pale.
Hawaendi na teknolojia, mitandao ya kijamii, au mabadiliko ya tabia za wateja.
Ni jambo gani ambalo bado unahitaji usimamizi kati ya haya?
Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
Share ujumbe huu kwa watu wengine ili kujenga biashara zao.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.