Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kansela Friedrich Merz 05.10.2025
Na:Cantona Joseph|RFA
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuendesha “vita ya mseto” dhidi ya Ujerumani.
Merz aliambia kituo cha televisheni cha NTV hapa Ujerumani kwamba kiongozi huyo anapigana vita ya taarifa dhidi yao, anapigana vita ya kijeshi dhidi ya Ukraine na vita hiyo inawalengo wao wote.Aidha Kansela huyo wa Ujerumani aliongeza kwa kusema Putin anataka kuipindua kabisa hali ya kisiasa ya Ulaya na ndiyo sababu wanaiunga mkono Ukraine.
Anasema kwa maslahi ya Ujerumani wanapaswa kulinda utaratibu wa kisiasa wa jamii zilizo wazi na huru barani Ulaya. Kansela Merz amesema kuwa alikuwa na mjadala mkali kuhusu suala hilo na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán katika mkutano wa Umoja wa Ulaya uliofanyika Copenhagen juma lililopita.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.