Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas
Na:Cantona Joseph|RFA
Duru ya kwanza ya mazungumzo kuhusu Gaza kati ya Hamas na wapatanishi imekamilika “katika mazingira chanya”, nchini Misri. Hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vinavyohusishwa na serikali ya Misri.
Al-Qahera News, chombo kinachohusishwa na ujasusi wa serikali, kiliripoti kuwa mazungumzo yataendelea, pia kati ya Hamas na wapatanishi katika mji wa mapumziko wa Sharm El-Sheikh, ambako ujumbe wa Israel uliwasili jana Jumatatu.Israel na Hamas wanatarajiwa kushiriki mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kubadilishana mateka na wafungwa pamoja na kusitisha mapigano kwa muda mrefu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.