Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Kama unaona dalili hizi katika biashara yako, hongera sana.
Hiyo ni ishara kuwa biashara yako inaanza kukua kwa msingi imara. Wekeza nguvu zaidi..
1. MAUZO YAKO YANAONGEZEKA TARATIBU
Ukiona wateja wanaongezeka, na mapato yako yanapanda hata kama si kwa kasi kubwa.
NINI CHA KUFANYA; Anza kuweka rekodi sahihi za mauzo ili ujue mwenendo wako.Tumia ongezeko hilo kupanga kuwekeza tena kwenye bidhaa au matangazo.
…
2. WATEJA WANARUDI TENA.
Wateja ambao unawahudumia walianza kurudi zaidi ya mara moja na wanawashawushi wengine na wanakuletea marafiki, hiyo ni dalali biashara yako inakua.
NINI CHA KUFANYA:Unda mfumo wa uaminifu tengeneza ofa au zawadi kwa wateja wa kudumu. Na boresha zaidi huduma nzuri.
Sikiliza mrejesho wao, malalamiko yao na fanyia kazi ndiyo silaha yako ya ukuaji.
…
3. UNAANZA KUPATA MAPENDEKEZO.( Referrals)
Wateja wako wanakutangaza bila wewe kuwaomba.
NINI CHA KUFANYA:Shukuru na thamini wateja hao, unaweza kutengeneza zawadi kwa wanaofanya hivyo, kwa kuwapa motisha ndogo kama punguzo au zawadi.
…
4. UNAANZA KUPATA CHANGAMOTO MPYA
Mauzo yanaongezeka, lakini pia unahisi presha mpya, muda hautoshi, unahitaji wafanyakazi, au mfumo bora zaidi,au mtaji hautoshi unahitaji kuongeza.
NINI CHA KUFANYA:Chukua hatua za kuandaa mifumo (systems) badala ya kufanya kila kitu mwenyewe, lakini kama changamoto ni mtaji Tafuta vyanzo vingine vya kupata.
..
5. BIASHARA YAKO INATAMBULIKA ZAIDI.
Watu wanaanza kukutaja, kukufuata kwenye mitandao, au kuuliza kuhusu huduma zako, au hata kukutafuta wao wenyewe.
NINI CHA KUFANYA:Boresha branding yako kama logo, maudhui, mtandaoni,. matangazo zaidi.Hakikisha huduma zako zinabaki bora usiharibu jina lako wakati wa kukua.
…
6. UNAPATA FURSA MPYA (Partnerships au Collaborations)
Watu wengine wanataka kushirikiana nawe kwa kuuza, kutangaza au kufanya miradi pamoja.
NINI CHA KUFANYA:Chagua fursa zenye faida na zinazolingana na maadili ya biashara yako.Usikubali kila ofa bila kufanya tathmini ya kina.
…
7.UNADHIBITI FEDHA ZAKO VIZURI ZAIDI
Sasa unajua pesa inatoka wapi na inaenda wapi. Unajua matumizi na Pato lako Unaweka akiba, na unajilipa kama mfanyakazi wa biashara yako.
NINI CHA KUFANYA:Tumia mfumo wa uhasibu, Tumia mifumo ya kukusaidia, kama Businesssoft, Kuza Business, thl app. Hizi zitakusaidia kutambua tofauti kati ya mapato, faida, na mtaji.
Ni dalili gani kati ya hizi 7 tayari naiona kwenye biashara yako?
Na ipi bado inakupatia changamoto?
Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.