Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kumaliza mzingiro

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vikosi vya serikali ya Somalia vimefanikiwa kumaliza mzingiro wa saa sita uliofanywa na wapiganaji katika gereza kubwa lililoko karibu na ofisi ya rais jijini Mogadishu, kwa kuwaua washambuliaji wote saba.

Vikosi vya usalama vya Somalia mjini Mogadishu
Vikosi vya usalama vya Somalia vikikagua eneo la shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari huko Mogadishu, Somalia Agosti 22, 2023.Picha: Abukar Muhudin/AA/picture alliance

Na:Cantona Joseph|RFA

Katika taarifa yake ya jana Jumapili, serikali ilisema hakuna raia wala maafisa wa usalama waliouawa katika makabiliano hayo ya Jumamosi, ambayo kundi la wapiganaji wa al-Shabaab lenye mahusiano na al-Qaeda lilihusika.Serikali ilisema hakuna mfungwa yeyote aliyeweza kutoroka kutoka gereza la Godka Jilacow wakati wa shambulio hilo.

Somalia imekuwa na utulivu kwa kiasi fulani katika miezi ya hivi karibuni, ambapo vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanamgambo wa ndani na wanajeshi wa Umoja wa Afrika, wakiwasogeza wapiganaji wa al-Shabaab kutoka maeneo kadhaa ya kati na kusini mwa Somalia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment