Unasema nini na watu wako wa karibu?

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Leo nimejiuliza swali, hivi mimi huwa najadili nini na watu wangu wa karibu?

Mwaka 1968 Bill Gates alikutana na rafiki yake Paul Allen ambaye walikuwa wanasoma darasa moja.

Siku moja wakiwa bado shuleni walikuwa wanasoma jarida la “Fortune Magazine” ambalo…

…lilikuwa linaelezea makampuni 500 makubwa duniani.

Bill Gates akamuuliza rafiki yake Allen…

“Hivi umeshawahi kufikiria jinsi ya kuendesha kampuni kubwa kama hizi zilizotajwa?”.

Allen akamjibu…

“Pengine siku moja tutakuwa na kampuni yetu ya Kompyuta Kubwa kama hizi”.

Hivi ndivyo safari ya kuijenga kampuni kubwa duniani ya MICROSOFT ilivyoanza.

Hivi ingekuwaje kama Allen angemcheka kuhusiana…

…na lile swali lilikuwa limejaa maono makubwa?

Mtu mmoja alisema watu wa CHINI hujadili WATU wengine…

Watu wa KATI hujadili MATUKIO…

Na watu wa JUU hujadili MAWAZO.

Je, wewe huwa unajadili mambo gani ukiwa/ukichat na rafiki zako?

Hebu angalia magroup yako ya WhatsApp yamejaa stori za WATU, MATUKIO au MAWAZO.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment