Uchaguzi umefanyika kwa usalama bila kuingiliwa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wajumbe wa uchaguzi wanahesabu kura huko Aleppo, Syria, Oktoba 5, 2025.

Na:Cantona Joseph|RFA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Syria, Noureddine al-Baba, amesema uchaguzi wa bunge nchini humo umekamilika katika vituo vyote vya kupigia kura bila tukio lolote la kuhatarisha usalama.

Akizungumza na shirika la habari la DPA, jana Jumapili, Noureddine al-Baba amesema wizara hiyo ilihakikisha usalama katika vituo vyote 50 vya kupigia kura vilivyotawanyika kote nchini, na kulinda zaidi ya maafisa 7,000 wa kamati ya uchaguzi.Al-Baba amesisitiza kuwa huo ni uchaguzi wa kwanza nchini Syria kufanyika bila kuingiliwa na vyombo vya ujasusi au maafisa wa serikali katika uteuzi wa wagombea, na kwamba mchakato huo umefanyika kwa uhuru.Syria imefanya uchaguzi wa bunge Jumapili hii kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Bashar al-Assad, hatua muhimu katika kipindi cha mpito cha taifa hilo baada ya takriban miaka 14 ya vita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment