Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Wanaume wawili wa jamii ya Kiyahudi wamefariki dunia huku wengine watatu wakilazwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya kufuatia shambulio la gari na kisu lililotokea mjini Manchester, Uingereza.
Shambulio hilo limetokea nje ya sinagogi katika siku ya Yom Kippur, inayotajwa kuwa siku takatifu zaidi katika kalenda ya Kiyahudi na limezua maswali kuhusu usalama wa jamii za wachache katika nyakati za ibada.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi wa Manchester, mshambuliaji aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama wakati wa tukio hilo, huku washukiwa wengine watatu wakikamatwa.
Taarifa ya polisi imeongeza kwamba wamemtambua mshambuliaji huyo kuwa Jihad Al-Shamie, raia wa Uingereza mwenye asili ya Syria, mwenye umri wa miaka 35.
Polisi imetangaza tuko hilo kuwa la kigaidi na wanaendelea na uchunguzi kubaini nia ya shambulio hilo.
Vikosi vya usalama vimeimarisha ulinzi katika maeneo ya ibada kote Uingereza.
Tutumie maoni yako
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.