Putin aionya Marekani kuhusu kuipa Ukraine makombora

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameionya Marekani kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo kati ya Moscow na Kyiv endapo Marekani itaikabidhi Ukraine makombora ya masafa marefu aina ya Tomahawk.

Akizungumza katika kikao cha majadiliano cha Valdai kilichofanyika mjini Sochi siku ya Alhamisi, Putin ameeleza kuwa hatua hiyo ya Marekani haitakuwa tu msaada wa kijeshi, bali itatafsiriwa kama ushiriki wa moja kwa moja wa kijeshi wa Marekani katika vita vinavyoendelea.

Putin amesisitiza hatari ya hali hiyo, akielezea uwezo wa makombora ya Tomahawk kuidhuru Urusi, na kuongeza kwamba hata iwapo Ukraine itapewa makombora hayo, haitabadilisha chochote katika uwanja wa vita.

Pia ameonya kwamba hatua hiyo inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya Urusi na Marekani.

Kauli ya Putin ameitoa katika wakati ambapo mataifa ya Magharibi yanatathmini uwezekano wa kuchukua hatua zaidi za kijeshi na kuiwekea vikwazo zaidi Urusi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment