Ukandamizaji unaozidi kutishia uchaguzi wa Octoba nchini Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, katika ripoti yake inaishtumu serikali ya Tanzania kwa kuminya uhuru wa kisiasa, hatua ambayo inatilia shaka iwapo uchaguzi mkuu wa tarehe 29 mwezi huu utakuwa wa huru na haki.

Rais wa Tanzania Samia Hassan na wafuasi wake wakati akichukua fomu ya kuwania urais.
Rais wa Tanzania Samia Hassan na wafuasi wake wakati akichukua fomu ya kuwania urais. © Ikulu ya Tanzania

Na:Cantona Joseph|RFA

Human Rights Watch katika ripoti yake, inasema serikali nchini Tanzania, imeendelea kukandamiza wanasiasa wa upinzani na wakosoaji wa chama tawala CCM, kuminya uhuru wa vyombo vya Habari, na kuingilia uhuru wa Tume ya Uchaguzi.

Nomathamsanqa Masiko-Mpaka, mtafiti wa Shirika hilo barani Afrika, amesema serikali ya Tanzania, inapaswa kuacha vitendo hivyo na badala yake kushiriki kwenye majadiliano na wapinzani wake, ili kuleta mageuzi muhimu, yatakayosaidia uchaguzi huo kuwa huru na haki.

Aidha, Shirika hilo linasema, limenakili visa 10 ambapo wapinzani wa serikali, wametekwa, kukamatwa na kuteswa kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa, akiwemo kiongozi mkuu wa upinzani Tundu Lissu ambaye alikamatwa mwezi Aprili, na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment