Kiongozi wa jeshi la Hamas huko Gaza apinga mpango wa kusitisha mapigano

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Izz al-Din al-Haddad anafikiriwa kuamini kuwa mpango huo uliundwa ili kuimaliza Hamas, iwe kundi hilo litakubali au la, na hivyo amedhamiria kupigana.

Na:Cantona Joseph|RFA

Israel imeendeleza mashambulizi yake katika mji wa Gaza tangu rais Trump kuzindua mpango wake wa amani

Wapatanishi wamewasiliana na mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza, ambaye alionesha kwamba hakubaliani na mpango mpya wa Marekani wa kusitisha mapigano.

Izz al-Din al-Haddad anafikiriwa kuamini kuwa mpango huo uliundwa ili kuimaliza Hamas, iwe kundi hilo litakubali au la, na hivyo amedhamiria kupigana.

Mpango wa vipengele 20 wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kumaliza vita ambao tayari umekubaliwa na Israel, unaeleza kuwa Hamas itaweka silaha chini na haina jukumu la baadaye katika kutawala Gaza.

Inadhaniwa kuwa baadhi ya uongozi wa kisiasa wa Hamas nchini Qatar uko tayari kuikubali kwa marekebisho, lakini wamepata ushawishi wao kuwa mdogo kwani hawana udhibiti wa mateka wanaoshikiliwa na kundi hilo.

Inaaminika kuwa kuna mateka 48 waliosalia, 20 tu kati yao wanaodhaniwa kuwa hai.

Kikwazo kingine kwa Hamas ni kwamba mpango unawahitaji kuwakabidhi mateka wote katika muda wa saa 72 za kwanza za usitishaji mapigano, kutoa suluhu lao pekee la mazungumzo.

Pamoja na hakikisho la Trump kwamba Israel itatii masharti hayo, kuna ukosefu wa imani ndani ya kundi hilo kwamba Israel haitarejelea operesheni zake za kijeshi mara itakapowapokea mateka, hasa baada ya kujaribu kuua uongozi wa Hamas huko Doha katika shambulio la anga mwezi uliopita.

Mamia ya wanaharakati washikiliwa na vikosi vya Israel baada ya meli ya misaada kuzuiliwa

Israel ilisema wote waliozuiliwa walikuwa "salama na afya njema"

Mamia ya wanaharakati, akiwemo mwanaharakati wa masuala ya hali ya tabia nchi wa Uswidi Greta Thunberg, wamezuiliwa na vikosi vya Israel baada ya kundi la ndege lililokuwa limebeba misaada kuelekea Gaza kuzuiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilisema wale wanaohusika na Global Sumud Flotilla (GSF) walikuwa wakihamishiwa katika bandari ya Israel ili wafukuzwe.

Boti za kwanza zilisimamishwa takriban maili 70 kutoka pwani ya Gaza katika maji ya kimataifa na nyingine karibu.

Israel imekuwa ikilinda eneo hili lakini haina mamlaka huko.

Israel ilisema jeshi lake la wanamaji liliambia boti hizo kubadili mkondo kwa kuwa “zilikuwa zikikaribia eneo la mapigano na kukiuka kizuizi halali cha wanamaji”, huku GSF ikielezea uvamizi huo kuwa “haramu”.

Kundi hilo lilisema jibu la Israeli “sio kitendo cha kujilinda”, lakini “kitendo cha kukata tamaa”. Inakadiriwa watu 443 walizuiliwa kutoka kwa boti na inadaiwa wengi walishambuliwa kwa maji ya kuwasha.

Israel ilisema wote waliozuiliwa walikuwa “salama na afya njema”.

Nchi kadhaa zimeelezea wasiwasi wake kuhusu tukio hilo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye alisema kuingiliwa kwa maji ya kimataifa ni “kinyume na sheria za kimataifa na kunakiuka uhuru wa kila taifa ambalo bendera yake ilipeperushwa kwenye meli kadhaa kwenye flotilla”.

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki ililaani uvamizi huo na kusema ni “kitendo cha kigaidi”, na kutoa wito kwa “wahusika wa shambulio hili” kuwajibika.

Rais wa Colombia Gustavo Petro amewafukuza wanadiplomasia wote wa Israel waliosalia nchini humo kwa kujibu, na kushutumu uvamizi huo kama “uhalifu wa kimataifa uliofanywa na [Waziri Mkuu wa Israel] Netanyahu”.

Petro pia alisitisha mkataba wa biashara huria wa Colombia na Israel, uliokuwepo tangu 2020, na kutaka kuachiliwa kwa Wacolombia wawili waliokuwa ndani ya flotilla.

Rais Samia ateua viongozi wapya wa taasisi za usimamizi wa mabasi yaendayo haraka

Basi liendalo kasi

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wapya katika taasisi zinazosimamia huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka imeeleza kuwa, Sais Tunda ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART).

Tunda anachukua nafasi ya Dkt Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia Rais Samia amemteua Pius Ng’ingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka (UDART), akichukua nafasi ya Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake pia umetenguliwa.

Hapo jana picha za video zilisambaa mitandaoni zikionesha baadhi ya vioo vya mabasi na vituo vikiwa vimevunjwa baada ya kushambuliwa kwa mawe usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni njia hiyo ya usafiri inayotegemewa na maelfu ya wakazi wa jiji hilo kubwa zaidi nchini Tanzania imekumbwa na malalamiko ya wananchi kutokana na uhaba wa mabasi ikilinganishwa na idadi ya abiria.

Hata hivyo jumatano asubuhi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo kikuu cha mabasi ya mwendo kasi na kuwaomba radhi watumiaji wa usafiri huo na kuwataka kuwa na subira wakati serikali ikiendelea na mipango ya kutatua adha wanazozipitia ikiwemo kuongeza idadi ya mabasi.

Watu wawili wauawa katika shambulio la sinagogi Manchester

.

Polisini mjini Manchester nchini Uingereza wamesema watu wawili wameuawa na wengine watatu wako katika hali mahututi kufuatia shambulizi lililolenga hakalu ya Wayahudi.

Idara ya polisi aidha imethibitisha kuwa mshukiwa mmoja aliuawa baada ya kupigwa risasi na polisi, lakini imekiri kuwa tambulisha kamili wa mshukiwa huyo hauwezi kuthibitishwa kikamilifu kutokjana na vitu alivyokuwa amebeba.

Picha iliyosambaa mitandaaoni imeonyesha mtu anayeshukiwa kutekeleza shambulio hilo akiwa na ndevu akiwa amevalia mavazi meusi akisimama nje ya sinagogi, huku akiwa amejifunga vitu visivyotambulika kiunoni huku akiwa ameshika kingine mkononi.

Waziri Mkuu wa uingereza Sir Keir Stammer amesema maafisa zaidi wa polisi watapelekwa ili kushika doria katika sinagogi kote nchini humo, ili kuwahakikishia Wayahudi usalama wao kufuatia shambulio hilo.

Shambulio hilo limejiri huku waumini wa Kiyahudi wakiadhimisha sherehe za Yom Kippur, siku ambayo inachukuliwa kuwa siku takatifu zaidi katika kalenda ya Wayahudi.

Sir Starmer anatarajiwa kurejea nyumbani mapema kutoka Denmark ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa wakuu wa mataifa ya Ulaya, ili kuongoza kikao maalum cha kamati ya kitaifa ya ulinzi.

Elon Musk awa mtu wa kwanza duniani kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 500

Musk

Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla Elon Musk amekuwa mtu wa kwanza kuwahi kuvuka thamani ya dola bilioni 500, ya utajiri wake, huku thamani ya kampuni ya magari ya umeme na kampuni zake nyingine ikipanda mwaka huu.

Utajiri wa tajiri huyo wa teknolojia ulifikia kwa muda mfupi dola bilioni 500.1 Jumatano alasiri saa za New York, kabla ya kushuka hadi takriban dola bilioni 499 baadaye siku hiyo, kulingana na Forbes.

Kando na Tesla, hesabu za ubia wake mwingine, pamoja na uanzishaji wa ujasusi wa bandia xAI na kampuni ya roketi ya SpaceX, pia imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

Mafanikio haya yanadhihirisha nafasi ya Musk kama mtu tajiri zaidi duniani, mbele ya washindani wake katika sekta ya teknolojia ya kimataifa.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes Billionaires Index, Larry Ellison, mwanzilishi wa kampuni ya programu ya Oracle, ndiye mtu wa pili tajiri zaidi duniani, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 350.7.

Shughuli za maziko zafanyika baada ya Takribani watu 30 kufariki dunia Ethiopia

Waombolezaji

Shughuli ya maziko inafanyika kufuatia vifo vya takribani watu 36 katika eneo la Amhara nchini Ethiopia.

Jukwaa lililojengwa katika Kanisa la Menjar Shenkora Arerti Mariam lilianguka waumini walipokusanyika kwa hafla ya kila mwaka ya kusherehekea Mt.Maria.

Inspekta wa polisi Ahmed Gebeyehu alisema huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka, akiongeza kuwa waliothibitishwa kuwa wamefariki walikuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 80.

Makumi ya watu wahofiwa kufariki dunia baada ya jengo la shule kuporomoka

Waokoaji wataanza kutumia vifaa vizito kusogeza slabu za zege

Hakuna “dalili za uhai” chini ya vifusi vya mabaki ya shule ya Indonesia iliyoporomoka ambapo watu 59 bado hawajulikani walipo, waokoaji wamesema.

Mamia ya wanafunzi, wengi wao wakiwa wavulana, walikuwa ndani ya shule ya bweni ya orofa mbili ya Kiislamu katika mji wa Sidoarjo ilipoporomoka siku ya Jumatatu.

Takribani wanafunzi watano walipoteza maisha na takribani 100 kujeruhiwa, maafisa walisema.

Watu 13 wameokolewa kutoka kwenye vifusi tangu juhudi za uokoaji zilipoanza, ingawa wawili walipoteza maisha hospitalini.

Shughuli za uokoaji zimekuwa na changamoto kutokana na muundo usio imara wa jengo hilo.

Siku ya Alhamisi, shirika la kukabiliana na majanga (BNBP) lilisema waokoaji wanaotumia ndege zisizo na rubani za joto walishindwa kutambua dalili za watu kuwa hai kutoka kwenye vifusi.

Familia zenye wasiwasi zinangoja shuleni, wengi wao wakilia lakini wakiwa na matumaini kwamba wapendwa wao bado wako hai.

“Natarajia habari njema zaidi, kwamba kaka yangu ameokoka,” Maulana Bayu Rizky Pratama, ambaye kaka yake mwenye umri wa miaka 17 hayupo, aliliambia shirika la habari la AFP.

“Natumai kaka yangu atapatikana hivi karibuni. Najisikia huzuni nikimfikiria kuwa yuko huko chini kwa siku nne.”

Ahmad Ikhsan, 52, aliiambia Reuters: “Ninaamini mwanangu bado yuko hai.” BNBP ilisema Jumatano kwamba watu 59 bado walikuwa wamenasa kwenye vifusi, ingawa idadi hii imebadilika sana katika siku chache zilizopita, na Suharyanto mapema alisema kuwa data daima “itakuwa inakinzana” katika “hatua za mapema” za janga.

Jengo hilo lilikuwa likijengwa wakati liliporomoka, na sakafu mbili za ziada zikiongezwa. BNBP baadaye ilisema kwamba msingi usio thabiti wa jengo hilo ulimaanisha kuwa hauwezi kuhimili uzito huu.

Wakala wa mji wa Sidoarjo anasema wasimamizi wa shule hawakupata vibali vya kuongeza sakafu zaidi kwenye jengo hilo.

Mamlaka za Uganda zakanusha kuwashikilia wanaharakati wa Kenya

Wanaharakati hao wa Kenya walikuwa wakisaidia kampeni ya Bobi Wine

Mamlaka ya Uganda imekanusha kuwashikilia wanaharakati wawili wa Kenya wanaodaiwa ‘kutekwa nyara’ jana Jumatano katika mji mkuu Kampala.

Mwanasiasa mkuu wa upinzani Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi Ssentamu kupitia akaunti ya X alisema wawili hao, Bob Nyagi na Nicholas Ayoo ‘walitekwa nyara na maafisa waliokuwa wamejihami’ wakiwa kwenye kituo cha mafuta na kupelekwa kusikojulikana.

Hata hivyo, msemaji wa polisi Uganda, Kituma Rusoke ameiambia BBC kwamba wanaharakati hao wawili wa Kenya hawako chini ya ulinzi wa polisi.

“Watu hao [Bob Nyagi na Nicholas Ayoo] hawako chini ya ulinzi wa polisi, wasiliana na chombo kingine chochote [shirika la usalama]”

Alipotafutwa na BBC, msemaji wa jeshi Felix Kulayigye alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu ni madai yanayowahusisha ‘watendaji wa usalama’ wasio na sare.

Pia alimpa Bobi Wine jukumu la kuthibitisha madai ya utekaji nyara na ni chombo gani cha usalama kiliyaendesha.

“Katika sheria wanasema, uthibitisho upo kwa mshitaki” alisema.

Lakini mashirika ya usalama ya Uganda mara nyingi yamekuwa yakishutumiwa kwa kupanga kukamatwa kwa wanasiasa na wafuasi wa upinzani huku wakiwa hawajavaa sare.

Baadhi mara nyingi hujitokeza tena mahakamani kwa mashtaka ya jinai.

Wakati huo huo kampeni za urais zinaendelea katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Bob na Nicholas walikuwa wameshiriki hivi karibuni katika mikutano ya kampeni ya Bobi Wine, ambaye anatafuta kumng’oa rais aliye madarakani Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa takribani miongo minne.

Viongozi mbalimbali watuma rambirambi kwa Jane Goodall

.

Vingozi mbalimbali duniani wameendeela kutuma risala zao za rambirambi kufuatia kifo cha Jane Goodall, mwanasayansi aliyegundua ukaribu wa sokwe na binadamu.

Rais wa Tanzania, ambako Goodall alisomea sokwe, amasema “kazi yake ya Hifadhi ya Kitaifa ya Gombe ilibadilisha uhifadhi wa wanyamapori.”

Utafiti huo “uliweka nchi yetu katika kiini cha juhudi za kimataifa za kulinda sokwe na asili,” Rais Samia Suluhu aliandika kwenye X.

Mwanmfalme Harry na mkewe Meghan walimsifu Goodall kama “mwanasayansi mwenye maono ya kibinadamu, mwanasayansi, rafiki wa sayari na rafiki yetu.”

“Ahadi yake ya kubadilisha maisha inaenea zaidi ya yale ulimwengu uliona, na pia kwa yale ambayo sisi binafsi tulihisi.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guttierez, alinukuliwa akisema katika X: Goodall anaacha “urithi wa ajabu kwa ubinadamu na sayari yetu,” “Nimesikitishwa sana kuhusu kifo cha Jane Goodall, Mjumbe wetu mpendwa wa Amani,” aliongeza, akirejelea nafasi ya heshima aliyoipata Goodall tangu 2002 katika shirika la kimataifa kwa kazi yake ya uhifadhi.

“Zaidi ya yote, Jane alitufundisha kwamba tunapotafuta ubinadamu katika ulimwengu wa asili unaotuzunguka, tunagundua ndani yetu wenyewe,” rais wa zamani wa Marekani Joe Biden alisema.

Mnamo Januari, katika siku za mwisho za uongozi wake, Biden alimtunukia Goodall Nishani ya Rais ya Uhuru — heshima ya juu zaidi ya kiraia katika taifa hilo.

UN yaidhinisha kikosi kikubwa zaidi kukabiliana na ghasia za magenge Haiti

.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kikosi kikubwa zaidi cha usalama cha kimataifa kwa ajili ya Haiti kukabiliana na ghasia za magenge zinazoongezeka katika nchi hiyo yenye migogoro.

Kikosi hicho kinachojulikana kama “Genge Suppression Force” (GSF) kitakuwa na hadi polisi na wanajeshi 5,550 wenye uwezo wa kuwaweka kizuizini washukiwa wa genge.

GSF itaongeza ujumbe wa Kimataifa wa Msaada wa Usalama unaoongozwa na Kenya (MSS) – kikosi ambacho kilikusudiwa kuwa na hadi wanachama 2,500, lakini kikakumbwa na upungufu mkubwa na kimekuwa na wakati mgumu kuzuia ghasia tangu kutumwa nchini humo mwaka 2023.

Zaidi ya watu 5,500 waliuawa katika ghasia zinazohusiana na magenge nchini Haiti mwaka wa 2024. Magenge yenye silaha kwa sasa yanadhibiti takriban 85% ya mji mkuu, Port-au-Prince.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment