Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kundi la Hamas limekanusha kuwa na uhusiano kwa namna yoyote ile na washukiwa waliokamatwa nchini Ujerumani kwa tuhuma za kununua silaha kwa lengo la kufanya mashambulizi dhidi ya raia wa Israel au majengo ya Wayahudi.
Kupitia taarifa rasmi, Hamas imesema kuwa madai ya kuwa na uhusiano na washukiwa hao ni ya uongo na kwamba yanakusudia kuchafua jina na harakati za kisiasa za kundi hilo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa tuhuma hizo zinalenga kupotosha raia wa Ujerumani ili kupunguza mshikamano wao na watu wa Palestina.
Hamas imefafanua kuwa sera yake inalenga kuendesha mapambano dhidi ya ukaliaji wa Israel ndani ya ardhi ya Palestina, na wala sio kushambulia raia katika mataifa ya kigeni.
Waendesha mashtaka wa Ujerumani walitangaza jana kuwa, wamewakamata washukiwa watatu wanaodaiwa kuwa wanachama wa Hamas mjini Berlin ambao wanatuhumiwa kununua bunduki kwa ajili ya kufanya mashambulizi dhidi ya raia wa Israel nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Alexander Dobrindt, ameielezea hali hiyo kama “tishio halisi,” na kusema kuwa Ujerumani imekuwa “eneo la oparesheni za magaidi.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.