Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waokoaji huko Java Mashariki, Indonesia wanakimbizana na muda ili kuwapata watu 38 wanaoaminika kuwa wamenasa kwenye vifusi vya jengo la shule ambalo lilianguka siku ya Jumatatu
Wanafunzi watatu wamefariki na wengine 99 walipelekwa hospitalini, baadhi yao wakiwa na majeraha mabaya, maafisa wanasema, na kuongeza kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
Wengi wa wale ambao wamenaswa ni wavulana ambao walikuwa wamekusanyika kwa maombi wakati jengo hilo lilipoanguka.
Jengo hilo la ghorofa mbili lilikuwa na msingi usio imara na halikuweza kuhimili uzito wa ujenzi wa ziada wa ghorofa mbili zaidi, maafisa wanasema.
Waokoaji wanajaribu kuwafikia manusura walionaswa chini ya kifusi – ambao baadhi yao bado wanaitikia – wakati familia zinasubiri kwa wasiwasi habari za wapendwa wao.
Maafisa wanasema kuna maeneo ambayo bado wanawasiliana na manusura – na wamewapa oksijeni, chakula na maji.
Operesheni ya uokoaji ilisitishwa kwa muda Jumanne, baada ya mamlaka kuonya juu ya jengo hilo kuanguka zaidi.
Wanafunzi walikuwa wamekusanyika kwa maombi katika Shule ya Bweni ya Kiislamu ya Al Khoziny, katika mji wa Java Mashariki wa Sidoarjo, wakati jengo hilo lilipoporomoka.
Mamlaka inasema shule hiyo haikuwa na vibali vya kupanua jengo lake.
Watu 69 wafariki katika tetemeko kubwa la ardhi Ufilipino

Takriban watu 60 wamefariki katika tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.9 katika kipimo cha Richter katikati mwa Ufilipino, wanasema maafisa wa usimamizi wa majanga.
Mji wa Bogo na miji mingine iliyoathiriwa wametangaza ‘hali ya maafa’ huku wakitathmini uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo.
Tetemeko la ardhi lilitokea kwenye ufuo wa Cebu City siku ya Jumanne na kusababisha kukatika kwa umeme na kuharibu majengo.
Taasisi ya Ufilipino ya Volcanology na Seismology haijatoa tahadhari ya kutokea kwa tsunami.
Wakaazi katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko wameiambia BBC kuwa walilala nje mitaani jana usiku.
Askofu mkuu wa Cebu amewaambia waumini kukaa mbali na makanisa. Wito huu ni muhimu kwani Cebu kilikuwa mojawapo ya visiwa vya kwanza vya Ufilipino kutawaliwa na Uhispania katika miaka ya 1500, na kina makanisa mengi ya zamani.
Mji wa Cebu, ilioko katika eneo la Visayas, ina wakazi karibu milioni moja.
Rais wa zamani wa Congo ahukumiwa kifo kwa uhalifu wa kivita

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila amehukumiwa kifo bila kuwepo mahakamani kwa uhalifu wa kivita na uhaini.
Mashtaka hayo yanamshutumu Kabila kuunga mkono kundi la M23, kundi la waasi ambalo limesababisha uharibifu katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Kabila alitiwa hatiani siku ya Ijumaa na mahakama ya kijeshi kwa uhaini, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na mauaji, unyanyasaji wa kingono, mateso na uasi.
Alikana mashtaka, lakini hakufika mahakamani kujitetea. Pia aliikataa kesi hiyo na kusema mahakama inatumiwa kama “chombo cha ukandamizaji”. Kwa sasa hajulikani alipo.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 54 aliiongoza DR Congo kwa miaka 18, baada ya kumrithi babake Laurent, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 2001.
Kabila alikabidhi madaraka kwa Rais Félix Tshisekedi mwaka 2019, lakini baadaye walitofautiana na akaenda uhamishoni mwaka 2023.
Mwezi Aprili mwaka huu, rais huyo wa zamani alisema anataka kusaidia kutafuta suluhu ya mgogoro katika eneo la mashariki na aliwasili katika mji unaoshikiliwa na M23 wa Goma mwezi uliofuata.
Rais Tshisekedi alimshutumu Kabila kwa nyuma ya M23 na maseneta walimwondolea kinga yake ya kisheria, na hilo kufungua njia ya kufunguliwa mashitaka.
Mapema mwaka huu M23 ilitwaa udhibiti wa maeneo makubwa ya mashariki yenye utajiri wa madini, ikiwa ni pamoja na Goma, jiji la Bukavu na viwanja viwili vya ndege.
Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa za Magharibi zimeishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono M23, na kutuma maelfu ya wanajeshi wake nchini DR Congo.
Lakini Kigali inakanusha mashtaka hayo.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya waasi na serikali yalifanyika mwezi Julai, lakini umwagaji damu umeendelea.
Serikali ya Marekani yafunga shughuli zake rasmi

Maseneta wa Marekani wameshindwa kupitisha mswada wa dakika za mwisho wa kuzuia kufungwa kwa shughuli za serikali, ambao ungehakikisha kuendelea kwa ufadhili wake.
Hii ni mara ya kwanza tangu 2018. Ingawa wafanyakazi muhimu wa serikali wataendelea na majukumu yao kama kawaida, lakini wale wanaoonekana sio muhimu watalazimika kwenda likizo bila malipo.
Huduma zitakazo athirika zaidi ni pamoja na mpango wa usaidizi wa chakula, shule za chekechea zinazofadhiliwa na serikali, utoaji wa mikopo ya wanafunzi, ukaguzi wa chakula na shughuli katika mbuga za kitaifa.
Rais Trump ametishia kupunguza bajeti ikiwa kufungwa huko kutatokea, na ametupa lawama zake kwa Wanachama wa Democratics.
Kufungwa huku kutawaacha maelfu ya wafanyakazi kwenye likizo bila malipo na kusimamishwa kwa programu na huduma nyingi za serikali.
Hili limekuja saa chache baada ya Seneti inayodhibitiwa na Republican kushindwa kupitisha mswada wa matumizi ya serikali.
Mbappe afikisha mabao 60 Ligi ya Mabingwa, aweka historia

Kylian Mbappe alifunga amefunga magoli matatu katika mechi moja na kufikisha mabao 60 kwenye Ligi ya Mabingwa wakati Real Madrid ilipoichabanga Kairat Almaty nchini Kazakhstan.
Nahodha huyo wa Ufaransa alipiga mkwaju wa penalti dakika ya 25 baada ya kipa Sherkhan Kalmurza kumchezea rafu Franco Mastantuono.
Aliongeza mabao bao la pili dakika ya 52 alipouunganisha mpira wa Thibaut Courtois na kuuzamisha nyafuni. Dakika ya 73 Mbape akaweka nyavuni goli la tatu.
Wachezaji wengine waliofunga ni E. Camavinga (83′) katika Brahim Díaz (90’+3)
Ulikuwa ushindi wa 5:0 ulikuwa muhimu sana kwa kikosi cha Xabi Alonso baada ya kufungwa 5-2 na wapinzani wao wa jiji la Atletico Madrid kwenye La Liga Jumamosi.
Mabao hayo ya Mbappe kwenye Ligi ya Mabingwa – yanamaanisha amempiku mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich Thomas Muller na kuwa mfungaji bora wa sita katika historia ya mashindano hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.