“The Goal” naye Dr. Eliyahu Goldratt

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Dr. Eliyahu Goldratt katika kitabu chake cha “The Goal” ameelezea nadharia ya…

Vipingamizi vya kutimiza malengo (Theory of Constraints – TOC)…

Ambavyo ukivijua vitakusaidia kujua mambo matatu muhimu:

1. Nini cha kubadilisha?

2. Ubadilishe kuelekea mwelekeo upi?

3. Ufanyaje ili upate mabadiliko unayoyataka?

Nadharia hii inalenga kuonyesha kuwa kutimiza malengo ambayo unayo…

Kama mtu binafsi ama taasisi ni zaidi ya kutumia vizuri rasilimali ulizonazo

Ni matokeo pia ya KUJUA VIKWAZO vinavyokukabili na kuweka MKAKATI MADHUBUTI wa kuvikabili kila siku.

Kupitia nadharia hii kwa utafiti alioufanya aliona unaweza kuongeza kipato chako kwa 68%…

Na unaweza kuongeza ufanisi wa matumizi ya muda wako hadi kwa 60%.

Unachotakiwa kufanya ni kujiuliza maswali Maalumu:

Hivi nini kinasababisha nishindwe kuweka akiba miaka yote hii?

Hivi kwa nini kila nikianzisha biashara ninafeli?

Hivi kwa nini watu muhimu wananikimbia baada ya muda?

Hivi mbona ninafanya kazi kwa bidii ila sioni matokeo yake? n.k

Kwenye zoezi hili fanya bidii kupata majibu mengi ya maswali yako uwezavyo.

Baada ya hapo jiulize – “Katika vikwazo Hivi vyote, ni Kipi ambacho ndio kinasababisha zaidi kunikwamisha?”.

Ukishakipata, weka mkakati kwenye maandishi wa kuanza kukabiliana nacho na UANZE LEO sio KESHO.

You Can’t CONQUER what you don’t CONFRONT (Huwezi kukishinda ambacho hauko tayari Kukikabili), Fanya Kitu Leo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment