USIDHARAU MAMBO HAYA 10 KAMA WEWE NI MFANYABIASHARA. YAFANYE MARA KWA MARA..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wengi wanataka mafanikio ila wanadharau vitu vitu hivi vya msingi. Weka umakini katika haya..

1.Kumtanguliza Mungu katika maisha yako

Biashara bila Mungu haina msingi imara. Toa sadaka, hudhuria ibada, omba na shukuru kila hatua. Kumbuka, si kila mtu anapenda mafanikio yako lakini Mungu akisimama nawe hakuna atakayekuzuia.

..

2.Tunza afya yako

Biashara inahitaji nguvu na akili timamu. Afya njema ndiyo msingi wa ndoto zako. Kula vizuri, kunywa maji ya kutosha, fanya mazoezi, na epuka mambo yanayoharibu mwili wako.

..

3 Usitoe siri za mafanikio yako hovyo

Sio kila jambo la kibiashara linahitaji hadhira. Weka siri zako za mapato, kodi, wauzaji wako na mikakati ya ukuaji. Siri zako ndizo nguvu zako.

4.Kuwa na nidhamu ya kifedha

Tenga pesa ya biashara na matumizi binafsi. Kutumia vibaya pesa ni chanzo kikuu cha kuua biashara. Haijalishi unapata kiasi gani bila nidhamu ya fedha, huna mafanikio.

5.Heshimu muda wako na muda wa wateja

Muda ni mtaji wa kipekee. Ukiheshimu muda wa wateja, utajenga uaminifu na heshima sokoni.

6.Jifunze kila siku

Biashara ni shule isiyo na mwisho. Sokoni mambo hubadilika kila saa. Hudhuria mafunzo, soma vitabu, tafuta maarifa mapya elimu ndiyo usalama wa biashara.

7.Toa huduma bora zaidi ya matarajio ya mteja

Huduma bora huwafanya wateja warudi tena na tena. Mteja mmoja mwenye furaha anaweza kukuletea wateja kumi zaidi.

8. Kuwa mvumilivu

Mafanikio makubwa hayaji mara moja. Yanahitaji bidii, maombi na uvumilivu. Kila siku unapopanda juhudi zako, unakaribia kuvuna matunda ya mafanikio.

9. Weka kumbukumbu za mapato na matumizi kwa uaminifu

Biashara bila hesabu ni safari gizani. Daftari lako ndilo kioo cha ukweli wa biashara yako.

10.Kuwa mbunifu na usiogope kubadilika

Soko hubadilika kila siku. Ukikataa kubadilika, biashara yako itasahaulika. Ubunifu ni injini ya ukuaji wa biashara.

Mafanikio ya biashara hujengwa juu ya tabia ndogo ndogo zinazofanywa kwa uaminifu kila siku.

Ni jambo gani unahitaji ufafanuzi zaidi.?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment